'Hakuna wapiga kura waliokufa wataibuka,'Ujumbe wa Akombe huku akimuomboleza Msando

EAkdgUQWwAAc7tS
EAkdgUQWwAAc7tS
Takriban miaka mitatu imepita tangu aliyekuwa meneja wa ICT wa IEBC Chris Msando kupatikana mwili wake umetupwa siku chache baada ya kuripotiwa kupotea.

Aliuliwa na mwanafunzi wa matibabu Caroline Ngumbu, familia yake iliadhimisha miaka mitatu jana tanhu kifo chake kutokea walichobaki na cho ni kumbukumbu tu zake.

Siku zimekuwa miezi na miezi kuwa miaka, hatimaye miaka mitatu imetimia tangu Msando afariki, alipatikana tarehe 28,Julai 2017 huku akiwa ameuawa.

"Kumbukumbu zako za kipekee zimesalia kwenye mioyo yetu, kwa hakika huwa tunakumbuka tabasamu yako, mienendo, hekima na ukarimu wako

Kumbukumbu zako hazitawahi zeeka maisha yako kwetu yalikuwa baraka tutakupeza milele, tunawaomba,jamaa,familia na marafiki kuombea moyo wake Chris kwa maana hatuwezi weka ibada ya wafu kwa ajili ya janga la corona

Lala salama shujaa wetu, kwa mikono yake Mungu umepumzika lakini utasalia mioyoni yetu milele."

Roselyn Akombe mwenzake mwendazake Msando naye alikuwa na haya ya kunakili ili kumkumbuka na kumuomboleza;

"Hakuna wapiga kura waliofariki wataibuka nikitazama-Chris Msando uchungu uliopitia miaka mitatu iliyopita wenzako walikupeleka kwenye chumba cha mauaji

Kama Judas walikuuza kwa sendi thelathini,tutapata haki yako hata kama itachua muda upi." Akombe Aliandika.