Hali tete wodi ya Ganda Malindi, Aisha Jumwa atoa tamko kuhusu zogo

a.jumwa__1
a.jumwa__1
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amefunguka kuhusu kisa cha jana jioni ambapo raia mmoja alipigwa risasi na kuuawa Malindi.

Haya yanajiri huku maafisa wa polisi wakichunguza kisa hicho.

Mauti ya Ngumbao Jola yalimkuta baada ya zogo kutokea katika mkutano wa ODM nyumbani kwa mgombeaji wa uwakilishi wodi ya Ganda, Reuben Katana.

"Mimi nakumbuka nikifika kwa huo mkutano. Nikishuka tu nilikutana na jamaa mmoja anaitwa Agunga. Na aliniambia mwacheni huyo mama aende atafanya nini na askari wote tunao wote..."

"So mi nikashindwa askari ni utumishi kwa wote na hawawezi kutake side..."

"Nataka niseme ya kwamba kitendo ODM wamefanya sio kizuri..."

"Wale waliopanga mkutano pale wakijua kwamba campaign period ilikuwa imeisha, wao ndio wanatakiwa wakuwe held responsible..." Alifunguka Aisha

Ghasia katika mkutano huu zilizuka Jumanne jioni.

 Ngumbao alipigwa risasi kwa bega na kufariki muda mchache alipofikishwa hospitali ya Malindi.

Marehemu Ngumbao Jola ni mjomba wa Katana.

Kufikia sasa haijabainika aliyefyatua risasi hiyo.

Kwa sasa viongozi wa ODM wakiongozwa na naibu gavana wa Mombasa William Kingi wamekita kambi nje ya lango za kituo cha polisi Malindi wakitaka Jumwa na genge la vijana waliozua rabsha kukamatwa.