Hamisa Mobetto ajidai kuwa anafanyaa vyema zaidi maishani kuliko Nandy

Screenshot.from.2019.10.17.16.25.49
Screenshot.from.2019.10.17.16.25.49

Binti Hamisa Mobetto kutoka Tanzania hana uhusiano mzuri na mwanamziki Nandy.

Akizungumza na vyombo vya habari,Hamisa alisema kuwa mwanamziki Nandy ajulikanaye  kwa wimbo wake 'Ninogeshe' alikosana naye vibaya baada ya tofauti kuibuka baina yao.

https://www.instagram.com/p/B2mH20llJ55/

Vilevile,Hamisa alisema kuwa, haoni haja ya kuzungumzia binti huyu kwani  hataki kuongea naye hata kidogo.

"I don't think we should talk about her. She has blocked me," Hamisa alisema.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa,ni heri wasizungumze kuhusu Nandy kwani Nandy anafanya vyema kwenye sekta yake na yeye anafanya vyema zaidi.

"It's better not to talk about her because there are more important things to talk about. She is doing good, I'm doing even better.''Hamisa alisema.

Hamisa alizidi kusema kuwa yeye hana kiburi na ndio maana anafanikiwa sana .

Kwa sasa, Hamisa anajaribu kuuza wimbo wa'Sensema' na pia anapanga kufanya kolabo na wanamziki wa kenya.

"We spoke about a collabo with Sauti Sol. It will be good and I also have a song with another Kenyan artiste," Hamisa alisema.