Hamstahili kupata hewa ya huru jaji wawaambia wauwaji sita

Crime scene
Crime scene
Wakati ndoa na familia inakuwa hufa hatari kwa mke, watoto huwauwa wazazi wao bila kupepesa macho, kuna kitu cha ubinadamu wetu kimepotea na lazima sheria itumike ili kutekeleza  na kueleza hofu yetu ya pamoja.

Haya yalikuwa maneno ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa walipokuwa wakiwatuma Ann Waithera, mtoto wake mvulana, shemeji yake na wafanyakazi katika mti wa mauaji ya David Macharia.

Waithera ni mke wa kwanza wa Macharia. Jaji Philip Waki, Roselyne Nambuye na Patrick Kiage walizingatia kifungo cha kifo kilicho pitishwa na mahakama ya juu kwa Waithera, Ruth Maina, David Kimotho, Joseph Kirumbi, Eliud Mwai na Joesph Maina wakisema kuwa walikuwa na haki na haria.

"Wahusika wa kitendo hicho hawapaswi kukubaliwa kupata hewa ya huru ama kutembea na uhuru katikati ya watu wanaojua maana ya maisha ya wenzio na kuwa na umoja," Benchi ilisema.

"Ni kwa wauaji wa moyo baridi adhabu ya kifo iliwekwa katika sheria na adhabu ambayo mahakama inapaswa kutangaza, ni sawa na yenye iliwekwa na hatuna sababu yeyote ya kuvuruga," tumethibitisha na kuizaingatia."

"Juni 12, 2004 Macharia aliamka kama kawaida na kuenda shambani mwake, usiku aliweza kulala kwa nyumba ya mke wake wa pili Hannah Wambui.

Waliishi katika kijiji cha Kamae, Kiambu katika shamba hilo alikuwa amemjengea mke wake wa pili Waithera.

Macharia alikuwa na watoto watano mmoja wao akiwa Joseph mtoto wa Waithera, uhusiano wao ulikuwa huendi sawa na hakuwai ishi katika nyumba ya mke wake Waithera.

Katika shamba hilo Macharia alikuwa anakamua ng'ombe na kisha kuenda kumalizia siku yake katika shamba na hakurudi tangu siku hiyo.

Wambui aliweza kuambiwa kisha kuenda kumtafuta, alienda katika mpwa wa mume wakwe na hakuweza kumpata huko baada ya siku tatu walienda kwa nyumba ya Waithera walipompata na msichana wake.

Waliweza kumuuliza aliko Macharia ilhali alisema lazima wamwambie kwanini wana mtafuta na kisha kusema hakuweza kumuona.

Majirani waliweza kusema kuwa Macharia alionekana akiwa anafuga  ng'ombe, hii iliweza kufanya familia kuwa na wasiwasi na kushuku kuwa Macharia amepotea kwa ajili ya kutoelewana na Waithera.

Macharia aliweza kumueleza ndugu yake vile Waithera alikuwa anawauliza wanawe kumchapa asipowatimizia mahitaji yao.

Wange mripoti kwa polisi kisha kuweza kushikwa na kupelekwa rumande, ambapo walimuumiza mkono wake na mtoto wake wa kwanza kumkata kidole na panga.

Polisi walipomtafuta Macharia nguvu zao ziliambulia patupu.

Siku moja Eliud alijitokeza na kusema ukweli, ambapo alisema kuwa waliweza kupewa pesa na dada yake Waithera, Wanjiru ili kuenda kuutupa mwili wa Macharia.

Baada ya wahusika hao kumuuwa Macharia walienda kumptupa kwa maji wakifikiria kuwa mwili huo hautawahi onekana milele.

Juni 24 polisi waliweza kuona gunia iliyokuwa katika mto wa Wagura, ndipo waliweza kuutoa mwili huo na kamba iliyokuwa imefunga mwili huo.

Katika gunia la kwanza palikuwa na mawe mzito, na gunia la pili palikuwa na mwili uliofungwa na blanketi kisha shingo yake ilikuwa na jeraha ya kina.

Wauaji hao waliweza kupewa adhabu ya kifo na mahakama ya juu na kisha kupinga na kupeleka kesi yao katika mahakama ya rufaa wakisema kuwa kulikuwa na makosa.