46153484_2227005214189643_5112363978205846507_n

Ushauri wa Mzee Kenyatta kwa manawe Uhuru Kenyatta kuhusu ndoa

NA NICKSON TOSI

Kwa mara ya kwanza rais Uhuru Kenyatta amebwaga manyanga na kusimulia jinsi alivyokutana na mama wa Taifa Margaret Kenyatta hadi wakawa mume na mke hadi leo.

Kwa miaka hiyo yote ambayo wawili hao wamekuwa kwa ndoa, hakuna ripoti za uzushi ambazo zimeripotiwa baina ya wachumba hao wawili.

Akiwa katika hafla ya Beyond Zero inayoongozwa na mama Margaret, Rais Kenyatta alisimulia jinsi rais mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta alivyomshauri baada ya kumuona Margaret kwa mara ya kwanza wakiwa wanaogelea kwenye kidimbwi [swimming pool].

Kulingana na Uhuru,Mzee alimuambia hivi.

‘Huyu anakaa mzuri,”Ushauri wa Mzee Kenyatta kwa Uhuru Kenyatta kuhusiana na Mama wa taifa Margaret.

Margaret Kenyatta

Rais Uhuru aliongezea kuwa uhusiano wake na Margaret Kenyatta uliimarika zaidi baada ya kuimarisha urafiki na ndugu wa Margaret walipokuwa katika shule ya upili.

Aidha rais alidokeza kuwa kuna wakati alianza kumtumia ujumbe Margaret ambaye ni mkewe kwa sasa  kupitia kitandawazi cha facebook hali iliyofanya uhusiano wao kuimarika zaidi.

The Kenyatta family

“Amekuwa rafiki na mfuasi wangu mkubwa, mwanamke ambaye ni mpole ,mnyamavu na hata wanangu wanaweza thibitisha hayo na pia ni mwanamke mwenye msimamo dhabiti,” aliongeza rais Kenyatta.

Uhuru and Margaret wedding

Kwa sasa wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya miaka 20.

 

Mhariri: Davis Ojiambo

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments