'Happy birthday kwa mke wangu wa pili,'Ujumbe wa baba wa kambo wa Diamond kwa Tiffah

Mwanawe msanii wa bongo Diamond na Zari Hassan Princess Tiffah amefikisha mika mitano hii leo Agosti,6,Tiffah ambaye anapendwa sana na mashabiki wake na kufahamika sana, alipata jumbe za wazazi wake na hata babu zake katika siku hii yake maalum.

Mama Dangote alikuwa na ujumbe huu wa kumwambia;

"DRAMA QUEEN LATIPHA NASEEB @PRINCESS_TIFFAH MTOTO MWENYE DRAMA ZAKE AFRICA 🌹❣ BIBI UWAA ANAKUPENDA SANA ZAIDI YA SANA." Aliandika Sandrah.

Mumewe Sandrah Rally Jones alimwandikia uumbe wenye mahabara tele huku akimtambulisha kama bibi yake wa pili kulingana tamaduni zao.

"Happy birthday kwa mke wangu wa pili @PRINCESS_TIFFAH 💓 🥰😍 kuwa na siku njema malkia wangu nakupenda sana dadake tee lock down kama lockdown inazuia kuja bongo."

Zari naye hakuachwa nyuma alimwamdikia mwanawe ujumbe huu;

"Hapo zamani muda mrefu mbali katika shamba la tegeta-magale, malkia alizaliwa na watu wa nchi hiyo walijawa na furaha kwa ajili ya kuzaliwa kwake
Na jina lake lilikuwa  @PRINCESS_TIFFAH Aliendelea kukua akiwa na neema machoni mwa watu na mwenye drama hadithi yake ni ya kushangaza na bado inaendelea HAPPY BIRTHDAY LIL MA🎂 💕 ALWAYS PRAYING FOR YOU🙏." Aliandika Zari.

Diamond naye alimwandikia haya;

"Happy birthday kwa mpenzi wangu wa maisha, maneno hayatoshi kueleza jinsi ninavyokupenda my Tee..@PRINCESS_TIFFAH ❤🌹❤."