Happy birthday Akothee! Tazama jinsi madam boss anavyosherehekea siku hii

Leo ikiwa Ijumaa tarehe kumi mwezi wa nne, ni siku ya kipekee Sana kwa wakristo wote duniani wanapoanza sherehe za pasaka.

Kukumbuka jinsi Yesu alivyopitia mateso mengi, akasulubiwa msalabani ili sisi tuokolewe dhambi zetu.

Vilevile, leo pia ni siku murwa kabisa kwa msanii madam boss Akothee ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Huku nchi nzima ikiwa kwenye kwarantini, madam boss alichukua fursa hii kuwakumbusha wafuasi wake kuwa walizaliwa na mikono miwili.

Mkono mmoja ni wa kujilisha na mwingine ni wa kulisha wasiojiweza.

Aliwashauri pia kuwa iwapo wangalijua umuhimu wa kusaidiana, hawangetaka kumuona yeyote akilala njaa.

Alisema hili huku akichapisha picha za vyakula ambavyo yeye na marafiki wake kutoka Akothee foundation, watakavyopeana kwa wasiojiweza.

Akothee aliandika :

HAPPYBIRTHDAY MIN JI

As you grow older , you will discover that you have two hands 🙏🏾

👉one for helping yourself, the other for helping others

🙏🏾 if you knew what I know about the power of giving , you would not let a single meal pass without sharing it in some way 🙏🏾

HAPPYBIRTHDAY MIN OYOO 🙏🏾🙏🏾🙏🏾