Happy birthday! Ghost Mulee asherehekea kuhitimu miaka 54

Kila mwaka siku ya kumi na saba, mwezi Julai, huwa siku ya kufana sana kwa mtangazaji Jacob 'Ghost' Mulee kwani ndio siku huadhimisha kuzaliwa kwake.

Kama ilivyo desturi, Mulee hupata fursa ya kukata keki pamoja na wafanyi kazi wenza na kusherehekea mwaka mwingine chini ya makali ya jua.

Mwaka huu, Ghost alipata zawadi kemkem na keki zimemngoja alipomaliza show yake ya Gidi na Ghost Asubuhi. Alizingirwa na marafiki na wafanyi kazi wenza akiwemo, Gidi Gidi.

Kwa furaha na vicheko vyake vya kuumiza mbavu, Mulee alikata keki akiadhimisha miaka 54 tangu azaliwe na kula na kila mmoja.

Kabla ya hafla hiyo fupi, mwenzake na boss wake, Gidi alimtumia ujumbe wa kusherehekea mafanikio yake huku akimtaja kama mwanaume kamili.

Gidi alimuombea mwenzake miaka nyingi na uzee ambao utamuacha kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars, bila meno.

Gidi alichapisha kwa mtandao wake wa Instagram akisema,

Let me take this earliest opportunity to wish this gentleman and colleague  a Happy birthday. May you grow to be toothless 😂😂😊

Mashabiki wa Mulee nao hawakusita ila kumuminia ujumbe wa heri njema.

paul.koskei: Happy Birthday Ghost. You guys promote a very natural platform on Radio for common Mwanainchi to air their views.

denniskayaviri: Happy born day coaches....may u leave to blow 100001 candles

njue_kami: Happy birthday day kicheko.. May u leave to blow 100001 candles..

ak1jcc1: Happy birthday to you, Ghost mzee wa kicheko

Sherehe hii yaja siku moja tu baada ya mtangazaji wa Mazungumzo waziwazi, Bramwell Mwololo pia kusherehekea siku ya kuzaliwa. Bramwell pia alipata fursa ya kukata keki pamoja na wafanyi kazi wenzake na marafiki kwa jumla.