Harambe stars yawasili nchini Kenya kutoka Misri

Timu ya taifa ya soka, Harambee stars imewasili nchini Kenya kutoka Cairo nchini Misri ilikokuwa ikishiriki michuano ya AFCON. Kenya iliwasili salama katika uwanja wa JKIA mwendo wa saa 3:30 asubuhi.

Hii ni kufuatia msururu wa matokeo duni kwenye michuano hio.

Kenya ilikuwa kwenye kundi C pamoja na Algeria, Tanzania pamoja na Senegal. Kenya ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lao hivyo kukosa nafasi kwenye raundi ya 16 bora.

Katika kundi C ambapo ilipoteza mechi mbili na kushinda moja. Algeria ilimaliza katika nafasi ya kwanza na alama tisa huku Senegal ikimaliza katika nafasi ya pili na alama 6.

Tanzania ilimaliza ya mwisho bila alama yoyote.