Harambee Stars wajikakamua na kutoka sare na wenyeji Misri

harambee stars
harambee stars

Harambee Stars jana walitoka sare ya 1-1 na wenyeji Misri katika mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2021.

Kenya walijipata nyuma ya the Pharaohs kufikia muda wa mapumziko kufuatia bao la Mahmoud Abdel-Moneim. Bao la kusawazisha la Kenya lilifungwa katika dakika ya 67 na Michael Olunga.

Mechi inayofuata ya Stars itakua dhidi ya Togo jumatatu uwanjani Kasarani.

Huenda Lionel Messi akachezea Argentina katika mechi ya kirafiki na Brazil nchini Saudi Arabia hii leo. Mahasimu hao wa Amerika Kusini watakutana jijini Riyadh huku Messi akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa tangu Julai.

Kiungo huyo wa Barcelona alipigwa marufuku ya miezi mitatu kwa kusema kuwa ligi ya Copa America ina ufisadi. Neymar hatacheza kutokana na jeraha la mguu lakini Gabriel Jesus yuko kwenye kikosi.

Uingereza walifuzu kwa Uro mwaka 2020 kwa kucharaza Montenegro mabao 7-0 ugani Wembley. Nahodha Harry Kane alifunga mabao matatu na kupanda hadi katika nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji mabao mengi, Uingereza, akiwa amefunga magoli 31 huku Alex Oxlade-Chamberlain, Marcus Rashford na Alexandar Sofranac wakifunga mabao hayo mengine.

Mshambulizi wa Chelsea Olivier Giroud alifunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti mabingwa wa dunia Ufaransa walipotoka nyuma na kuwanyuka Moldova 2-1 katika mechi yao ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 na kupanda hadi kileleni mwa kundi H.

Kufuzu kwa Ufaransa kulijiri kabla ya mechi hio kuanza kutokana na Uturuki kutoka sare na Iceland. Vadim Rata walifungia Moldova dakika tisa baada ya mechi kuanza kabla ya Raphael Varane kusawazisha na Giroud kufanya mambo kuwa 2-1.

Cristiano Ronaldo sasa amesalia na mabao mawili awe na jumla ya mabao100 katika mechi za kimataifa baada ya kufunga mabao matatu jana dhidi ya Lithuania katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2020.

Ureno ilishinda mechi hiyo mabao 6-0. Kiungo huyo wa Juventus mwenye umri wa miaka 34 huenda akawa mchezaji wa pili kufikisha mabao 100 ya kimataifa iwapo atafunga mabao mawili dhidi ya Luxembourg jumapili.

Manchester United ina nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Norway Erling Haaland kinda wa miaka 19, ambaye alifunzwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa Molde. Wakati huo huo United inatarajia kuafikiana na Juventus kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33, kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi ujao kabla ya uhamisho wa Januari.

Kiungo wa AFC Leopards Moses Mburu ameeleza kufurahishwa na kuregelea mazoezi na timu yake baada ya kukaa nje kwa takriban mwaka mmoja akiuguza jeraha.

Mlinzi huyo alifanyiwa upasuaji mwezi Septemba mwaka uliopita na kuregelea mazoezi miezi minne baadae kabla ya kupata jereha la mguu. AFC Leopards iko katika nafasi ya saba katika ligi ya KPL wakiwa na alama 15 baada ya mechi 9. Wtakabana na Bandari mjini Mombasa alhamisi wiki ijayo.

Kocha wa Chemelil Sugar Francis Baraza ameteuliwa kama kocha mkuu wa timu ya Tanzania Biashara United Mara. Baraza ameondoka Chemelil Sugar, ambao wako katika nafasi ya mwisho katika jedwali la KPL na hawajashinda mechi hata moja tangua kuanza kwa maimu mpya.

Alijiunga na timu hiyo Mei mwaka 2018 na ameshawahi pia kufunza Muhoroni Youth, Sony Sugar na Western Stima.