Harambee Stars yanyukwa na Senegal

stars
stars
Matumaini ya Harambee Stars kufuzu kwa awamu ya 16 katika makala ya 32 ya kombe taifa bingwa barani Afrika yalididimizwa jana baada ya kulazwa na Senegal mabao 3-0 katika uwanja wa Air Defence nchini Misri.

Matumaini ya Kenya kufuzu kwa awamu hiyo sasa yanategemea matokeo ya Mali na Cameroon wanaotarajiwa kucheza dhidi ya Angola na Benin mtawalia.

Harambee Stars watakuwa wanaomba Angola na Benini walio na alama mbili kila mmoja wapoteze mechi zao za leo za makundi.

Stars waliomaliza mechi na wachezaji 10 uwanjani baada ya Philomena Otieno kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, walikosa kuhimili msukumo wa Senegal katika kipindi cha pili huku Sadio Mane akipachika wavuni mabao mawili na moja la Ismael Sarr.

Penalti ya kwanza iliochanjwa na nyota wa Senegal Sadio Mane aliokolewa na mlindalango wa Harambee Stars Patrick Matasi ambaye alikuwa amethibiti lango na kupangua kila shambulizi la Senegal katika kipindi cha kwanza.

Senegal waliomaliza wa pili katika kundi C nyuma ya Algeria watachuana na Uganda.