Harmonize atikisa Dar Es Salaam, akosa kumtaja Diamond ngoma ya Uno

Screenshot_from_2019_12_09_05_03_16__1575885835_38484
Screenshot_from_2019_12_09_05_03_16__1575885835_38484
Msanii wa kizazi kipya Harmonize amelifunga tamasha lililofanyika uwanja wa Uhuru jiji la Dar Es Salaam.

Hafla hii ilikuwa imekusanya watu wengi wanaopenda burudani nchini humo.

Katika mistari wa ngoma yake ya Uno, Harmonize hakuimba kipande na ambacho alimtaja Diamond Platnumz.

Uhasama unaoekana kuwa bado upo baada ya Harmonize kiutema lebo ya WCB.

Hii ilikuwa mara ya kwanza Harmonize kutumbuiza katika jukwaa moja na Ali Kiba.

Ma-promota wa fiesta hiyo walikuwa tayari washatangaza kuwa mastaa hawa watakuwa katika ukumbi huo.

Tangazo la fiesta linajiri hii siku chache baada ya Harmonize kumaliza ubishi na mtayarishaji muziki hapa nchini Magix Enga.

Mkwaju huu ulikuwa ushaanza kupata upigwaji mkubwa redioni hapa nchini na kushika nafasi za kwanza katika mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe kuwa Harmonize alikuwa amefanya ziara kubwa Afrika mashariki akipigia Uno kampeni kubwa.

Ina maana kuwa meneja wake alifanya mazungumzo na kuridhiana na Magix Enga.

Zamani kipindi na amabapo Konde Boy alikuwa WCB, tamasha kama hili la kukutana na Alikiba halingefanyika.

Kima cha hela alichodaiwa na lebo ya Wasafi ni takriban milioni Tsh 5OO ili apate umiliki wa jina lake na ngoma.

Je, unaamini kuwa Harmonize bado ana uhasama na WCB?