vivian musician

‘Harusi bado ipo!’ Msanii Vivian apasua mbarika

Mwanamziki Vivian amepinga madai kuwa kuna shida ndani mwa ikulu yao na mpenziwe Sam West baada ya wawili hao kuahirisha harusi yao.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee ya moja kwa moja, msanii huyo wa ‘Chum chum’ alisema kuwa kukosana au kutoelewana kati ya wapendanao ni jambo tu la kawaida.

Jaguar alikuwa mshauri wangu, Vivian asema

 

Upande wake, Sam West, alisema kuwa harusi yao bado ipo na haijavunjiliwa mbali huku akisema kuwa sababu za kuiahirisha ni kwa sababu alimpoteza babake mpendwa na alikuwa anaipa familia yake mda ili ipone kutokana na msiba huo.

Anasema kuwa mapema 2020 yeye na mpenziwe Vivian watafunga ndoa katika harusi ya kizungu.

Mwaka uliopita, wawili hao walifanya harusi la kitamuduni ambayo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu na familia kutoka pande zote mbili.

Pata uhondo wote kutokana na mahojianohayo hapa

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments