Harusi ipo! Mamake Diamond Platnumz afichua siri

mama dangote
mama dangote
Mamake Diamond Platnumz Sanura Sandrah almaarufu kama mama Dangote amesema kuwa harasu ya mwanawe na mwana mitindo wa Kenya Tanasha Donna ingali ipo.

Diamond na Tanasha walitarajiwa kufunga pingu za maisha Februari katika siku ya wapendanao kabla ya kuiahirisha.

Kutoka wakati huo, wawili hao hawajazungumzia mipango hiyo lakini mama Dangote sasa ameamua kufunguka kuhusu harusi hiyo.

Alipoulizwa kuhusu harusi hiyo alisema;

HIO IPO.

Diamond amepaniwa kuweka sherehe kubwa ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mamake na mpenziwe hii leo kwani wawili hao walizaliwa siku moja. Sherehe hiyo imeitwa Gatsby 707.

Diamond alisema haya,

I FEEL SO GOOD. I NEVER THOUGHT I’D MEET SOMEBODY WHOM WE SHARED A BIRTHDAY TOGETHER. I FOUND OUT JUST THE OTHER DAY WHEN WE WERE SHOOTING THE CLIPS. THE IDEA WAS ALL TANASHA’S. SHE WANTED A GATSBY PARTY, YOU KNOW SHE IS HALF WHITE HALF BLACK.

Mama Diamond aliongeza kuwa mwanzo alimuona Tanasha kwa mitandao ya kijamii kabla ya mwanawe kumjulisha kwake.

Nilianza kuona picha hata kabla nikutane naye. Halafu akaja nyumbani. Alikuwa na uwoga mwingi. Sijui mbona.