Hassan Joho kuwania urais mwaka wa 2022

Photo source: kenyan-post.com

Gavana wa Mombasa Hassan Joho amesema atagombea wadhfa wa urais mwaka wa 2022.

Joho amesema taifa linafaa kujitayarisha kwa rais wa kwanza kutoka pwani, huku akiishtumu serikali ya Jubilee kwa kuendeleza uongozi wa maeneo mawili ya taifa. Ameishtumu serikali kuu kwa kujaribu kuchukua sifa za ustawi uliotekelezwa na serikali za kaunti.

Joho amesema mradi wa shilingi bilioni 200 wa kuimarisha mitaa ya Mombasa utaendelea licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya viongozi.

Hayo yakijiri, Gavana wa kakamega Wycliffe Oparanya anamtaka seneta wa Bungoma Moses Wetangula kutupilia mbali azma yake ya kuwania urais ili kumpa Raila Odinga nafasi hiyo. Oparanya amedaiwa kuwambia Wetangula kwamba iwapo ataendelea na jitihada za kutaka kuwa mgombeaji wa urais, basi asizindue mpango huo katika kaunti ya Kakamega.