HAT TRICK? Jamaa akiri kufanya MAPENZI na Mama na Nyanya ya mchumba wake.TAABU!

Otii 1 (1)
Otii 1 (1)
Josephat Otii*  anasumbuka fikra  kuhusu jambo ambalo  amekuwa akilifanya kwa muda bila kujua kwamba wakati mmoja litamweka mashakani . Lakini sasa ,yupo katika njia panda asijue la kufanya  na ameamua kuzungumza ili kutafuta usaidizi na ushauri ambao utamtoa katika   tatizo hili .Otii ,ameamua kufunga ndoa na mchumba wake wa miaka mitatu lakini kuna tatizo- mewahi kushiriki mapenzi na mamake mchumbake na pia kufanya hivyo na nyanyake mchumba wake!

Yote ukiyasikia ni kama filamu ya kinigeria lakini ukimwangalia usoni anapoyoa masimulizi yake na jinsi alivypozongwa na fikra ,basi utafahamu kwamba ‘This is an  emrgency’. Baada ya kuanza uhusiano na mchumbake Rebbeca wakiwa wote shuleni,kila kitu na mipango yao ilikuwa swafi na hatma yake ilionekana kuwa ndoa . Otii anasema ‘Becca’ kama  anavyomuita kiufupi ni  msichana mrembo na mkarimu na mwanamume yeyote angependa kuwa katika uhusiano wa kudumu naye .Baaada ya uhusiano wa  mwaka mmoja  na kumaliza masomo wote ,kila mmoja  alipata kazi na wakaaza kufikiria kuhusu jinsi  ya kuanza kuishi pamoja lakini mwanzo ,suala la kutambulishana kwa familia zao likaibuka .

Hapo  ndipo masaibu yalianza kumpata Otii kwa sababu walipanga kwanza kwenda kumtemeblea mamake Rebbeca  anayeishi mtaani Ngong ,Nairobi .Mamake Rebbeca  na biniye  wanafanana kama shilingi na nyingine na ukiwaona kwa mara ya kwanza ,uwezo wa wewe kufikiri ni mtu na dadake ni wa asilimia 100.  Katika umri wake ,mamake Rebbeca amejitunza  kwa njia ya kipekee na hata uhusiano kati ya mtu na binti yake sio kama wa mama na mwanawe bali kama wa rafiki wa karibu wa pamoja .Otii anakumbuka jinsi alivyotambulishwa kwa  mama mkwe mtarajiwa na alivutiwa sana na ucheshi wake na mtindo wake wa mavazi .

Mkutano wa kwanza ulikuwa mzuri ,mlo ukaandaliwa na  wapenzi hawa wawili wakamsimulia mama safari yao ya mapenzi na jinsi wanavyopanga kuishi kama mume na mume katika kipindi kifupi kijacho .Mama Rebbeca alionyesha furaha sana na wakati mwingi alikuwa akimhakikishia bintiye kwamba iwapo Otii ndiye aliyemchagua kama  mume mtarajiwa basi hakuwana pingamizi . Wiki mbili baada ya  kukutana na mama mkwe mtarajiwa , Otii alpigiwa simu na mwanadad mwenye sauti nzuri ya kuvutia,akamjulia hali na alionekana kufahamu kila chote kuhusu maisha yake.So, alichojiambia ni kwamba huyu ni mtu ambya elabda walisoma naye au rafiki wa zamani anajaribu kumfanyia sherehe kwenye simu kwa hivyo  he played along  hadi wakati  mwenzake upande wa pili alipojitambulisha kama mamake Rebecca ! Otii ,aliduwazwa asijue atasema nini zaidi ya hapo lakini ufupi wa kisa ni huu,mamake mchumbake aliconfess jinsi anavyompenda Otii na angependa fursa ya ‘kumjua kwa undani zaidi’.‘After all unamwoa binti yangu so I need to know who you are and what you stand for’.Alisema mamake Rebbeca .Kilele cha mchezo huu ni Otii alijipata wakati mmoja  amelala na   ‘mama mkwe matarajiwa’  , lakini sakata yake ndio ilikuwa imanza kushika moto kwani mengine yalikuwa yamemngoja njiani.

Uhusiano kati ya Rebbeca na Otii ulieelea kama kawaida ,pembeni Otii alikuwa akijutia kimoyoyo kuhusu alichokifanya na mama Rebbeca na disemba  ya mwaka jana yamemfika makubwa mabyo bado hajapata ufahamu ya mukhtasari wake . Mtu na mchumbake walimua kwamba likizo ya disemba basi watakwenda mashambani alikozaliwa Becca ,Nyahururu.Aliyeishi huko ni Nyanyake Becca ,mwanamke wa miaka 60 hivi ambaye alikuwa na ukakamavu wa kukataa  kabisa kuitwa nyanya .Hawana najua mnawafahamu sana   ‘nyanya dotcom’.Wanapiga  weave kwenye kichwa ,au nywele zinapigwa rangi na wakati wote ngozi wameilanisha kwa mafuta .Muonekano kila wakati ni kukataa kusalimu umri kuhusu matakwa ya umri .Mnawajua !

Mkesha wa krisimasi wakati  Rebbeca alipokuwa amejiacha ovyo -mtoto wa kike alipiga kileo kikamzidi nguvu na  akatekwa na usingizi.Otii pia alikuwa mlevi na hakujifahamu katika  chumba walichokuwemo . Ufupi ni kwamba  alipoamka mwendo wa kumi alfajiri alijipata katika chumba cha Nyanyake Rebbeca ,akiwa uchi kama alivyozaliwa! Ishara zote alizoweza kuzikumbuka ni kwamba walishiriki mapenzi .Hajui alivyofika chumbani mwa nyanyake mtu lakini anachokumbuka ni  wote watatu wakipiga stori kweli kweli usiku huku nyanya mtu akiwa halewi .Makubwa haya na sasa yote yamemjaa fikra Otii.Unajinasua vipi katika sarakasi kama hizi?