'Hata kitandani bananeni hamna corona,'Magufuli awaambia watanzania

Rais wa nchi ya Tanzania John Pombe Magufuli amezidi kuzungumzia hali ya virusi vya corona nchini Tanzania huku akiwaambia wananchi wa Tanzania kuwa hamna corona nchini humo.

Kupitia katika ujumbe wake akifanya kamapeni yake aliwaacha walihudhuria mkutano huo kwa kicheko baada ya kuwaambia wanandoa kuwa wanapaswa kubanana kitandani kwa maana hamna corona.

https://twitter.com/MasoloMabonga/status/1291610564653993986

Katika video iliyoenea sana kwenye mitandao ya kijamii Magufuli aliwaambia watanzania wanapaswa kukumbatiana hadharani na hata kitandani kwa maana Mungu amewawezesha kushinda virusi hivyo.

Kiongozi huyo ni mmoja wa viongozi barani Afrika baada ya kutoweka kanuni kama kafyu ama kutopiga marufuku kuingia kwa raia wa kigeni nchini humo.

Mwishoni mwa mwezi wa juni, Magufuli alifungua shule zote na hata kurejesha uchumi wa nchi hiyo.

Ni video ambayo ameibua hisia mseto kwa wanamitandao.