Hata mungu ashuke siwezi lea mtoto wa mama mwingine - Rosemary

Bi Rosemary alimuacha mtangazaji Massawe Japanni na waskizaji wa Radio Jambo vinywa wazi.

Hii ni baada ya kudai kuwa hawezi lea mtoto wa mama au mwanamke mwingine na kama atalazimishwa kufanya vile, basi watoto hao atawageuza vijakazi wake.

Alisema hawezi lea mwana wa mama mwingine kama mamake mzazi yu hai na kuwa kama ni kijana yeye ndiye atamlishia ng'ombe, na kama ni msichana yeye ndiye atamfanyia kazi za nyumbani.

Rosemary alisema kuwa hata mungu ashuke hivi leo, hana haja ya kuwa msafi mbele ya mungu kwani hata na dawa hawezi lelea mwanamke mwingine mtoto.

Soma usimulizi wake.

Massawe wacha nikuambie ukweli, mtoto mwenye amezaliwa mimi nikiwa na mwanaume mimi siwezi lea. Na nikilazimishiwa atakuwa maid (house help) na akiwa kijana nina ng'ombe atanichungia.

Mtoto mwenye nimepata naye mwanaume huyo namlea.

Siwezi lea kwa sababu mamake ako uhai kwani unajua unaweza kataa halafu ulazimishiwe uambiwe ni lazima utamlea, na hapo ndio nitafanya uamuzi wengi.

Mimi siwezi hata mungu akishuka hapa siwezi wacha tu niwe mbaya mbele ya mungu.