Islamic State
Kundi hili ambalo pia hujulikana kwa kiarabu kama Daesh au majina ya ufupisho ya ISIS na ISIL, lilikuwa hatari zaidi katika miaka mitatu iliyopita kabla ya kupunguzwa makali na juhudi za pamoja za Marekani na washirika wake na makundi mbali mbali ya wapiganaji wanaovisaidia vikosi vya usalama vinavyopambana na ugaidi katika mataifa ya Iraq na Syria . Kundi hilo liliyaenga pia mataifa yalio mbali na mashariki ya kati kama vile barani uropa na Asia .
Mashambulzi mengi ya ISIL yalikuwa ya mabomu .pia kundi hilo lilishiriki utekaji nyara wa watu na mauaji ya kuwakata watu shingo. Kwa sasa hata hivyo makali yake yamedidimia baada ya kuuawa kwa kiongozi wake wa kwanza Al baghadadi .
Taliban
Kundi hilo lenye chimbuko lake nchini Afghanistan limekuwa katika vita na majeshi ya muungano yanayoongozw ana marekani tangia mwaka wa 2001 na limesalia na nguvu za kusababisha maafa katika sehemu nyingi za mashariki ya kati . kudikia katikati ya mwaka wa 2017 kundi hilo lilikuwa likithibiti asilimia 11 ya sehemu ya ardhi ya Afghanistan na lilikuwa likilumbaia asilimia 29 ya wilaya 398 za taifa hilo . Kundi la Taliban linendelea na oparesheni zake katika asilimia 70 ya mikoa ya Afghanistan .
Al-Shabaab
Kundi hilo la kigaidi lilichipuka mwaka wa 2006 . Limejitambua kama sehemu ya mtandao wa kigaidi wa al qaida na linahudumu nchini Somalia lakini pia limefanya mashambulizi ya kila mara katika mataifa ya Ethiopia, Kenya na Uganda. Al shabaab lilikuwa kundi hatari zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka wa 2017.Thuluthi mbili ya vifo vilivyosababishwa na mshambulizi ya al shabaab vimetokea katika mji mkuu wa Soalia ,Mogadishu . kisa kibaya zaidi kilitokea mwaka wa 2017 oktoba wakati watu 588 walipouawa na wengin zaidi ya 316 kujeruhiwa .
Boko Haram
Kundi hilo lenye makao yake nchini Nigeria pia linafahamika kwa jina lake la kiarabu (Jama’tu Ahlis Sunna Lidda’awati wal-Jihad) na wakati mmoja lilikuwa hatari zaidi duniani lakini uwezo wake umekuwa ukididimia tangu mwaka wa 2014 na hivi maajuzi limegawanyika katika makundi madogo madogo . Tangu lilipochipuka kaskazini mashariki mwa nchi hiyo mwaka wa 2002 , Boko haram pia limesambaa hadi katika mataifa ya Chad, Cameroon na Niger na limesema linaunga mkono kundi la Islamic State . Mashambulizi mengi ya kundi hilo yalitekelezwa nchini Nigeria katika Jimbo la Borno ,huku visa vichache vidogo vikitekelezwa katika nchi jirani za Cameroun na Niger .Kundi hilo limelaumiwa kwa visa vingi vya utekaji nyara watu na kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga .
Makundi mengine ya kigaidi
Kando na makundi haya manne ya kigaidi kuna mashambulizi mengi ambayo hutekelezwa na vikundi mbali mbali likiwemo kundi la al qaeda.Mwaka wa 2019 makundi 169 yalihusika na takriban kifo kimoja lakini ni makundi 130 yaliyotekeleza mashambulizi hayo. Mengi ya makundi haya ni madogo lakini makubwa kama vile al qauda yana wapiganaji takriban elfu 30 katika mataifa 17 ya mashariki ya kati na afrika. Nchini Syria kuna makundi kadhaa yakiwemo Hayat al-Tahrir al-Sham (Awali yaliyojulikana kama Jabhat Fateh al-Sham na Al-Nusra) na Jaysh al-Islam. Nchini Pakistan makundi yaliyotambulika kwa kusababisha maafa kupitia mashambulizi ni pamoja na Lashkar-e-Jhangvi na the Khorasan Chapter linalohusiana na Islamic state . Katika taifa jirani la India kundi hatari zaidi ni la chama cha kikomunisti (Maoist) kwa jina jingine Naxals, ambalo lilisababisha vifo 205 kupitia mashambulizi 190. Mwaka jana makundi matano tofauti yakiwemo Lashkar-e-Taliba, Jaish-e-Mohammad na Hizbul Mujahideen, yalisababisha vifo vya watu 102. Thamani ya mali iliyoharibiwa kwa sababu ya vitendo vya kigaidi mwaka wa 2017 pekee ilikuwa dola bilioni 52.