Hatima ya Allan Omondi aliyetwangwa na polisi maandamano ya JKUAT

Kero la maafisa wa polisi liliwakasirisha watu wengi juma lililopita.

Wanapolisi walitumia nguvu kupita kiasi kukomesha maandamano katika eneo la Juja viunga vya mji wa Nairobi.

Hii ilipelekea maafisa hao kusimamishwa kazi zao za mamlaka ya kudhibiti na kuchunguza maafisa wa polisi (IPOA)

Ila Je, hatima ya kijana aliyeonekana akitwangwa viboko na maafisa wa polisi maandamano ya JKUAT imefikia wapi?

 Kijana huyu kwa jina Allan Omondi aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana katika video iliyotamba kwenye mitandap akipata kichapo hatari kutoka kwa maafisa wa polisi.

Hatima ya Allan Omondi aliyetwangwa na polisi maandamano ya JKUAT

Allan Omondi ni mwanafunzi wa somo la sayansi ya vyakula na teknolojia katika chuo hicho.

Allan alivumilia kichapo kikubwa sana na baadaye akazuiliwa katika kituo cha polisi.

Mama Allan alikuja alifika na kumchukua mwanawe.

Wanafunzi wale wengine waliachiliwa huru baadaye.

Allan alipelekwa Nairobi Hospital na hatimaye nyumbani kwao.