Hatima ya Russia kushiriki katika mashindano ya olimpiki kubainika Novemba

skysports-russia-olympics-athletics_4946081
skysports-russia-olympics-athletics_4946081
Hatima ya taifa la Urusi ama Russia ya kushiriki katika michezo ya Oilimpik itabainika kati ya Novema 2-5 mwaka huu.

Urusi ilikuwa imewasilisha kupinga hatua ya bodi ya World Anti-Doping Agencey WADA ya kuipiga marufuku ya miaka minne kutokana na hatua ya ongezeko la wanariadha wake kuendelea kutumia dawa za kusisimua misuli.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa mahakama ya kusuluhisha mizozo ya michezo almaarufu kama Court of Arbitration for Sports CAS, Shirikisho la Riadha la Urusi limetangaza kupinga hatua hiyo.

 Baadhi ya marufuku ambayo yaliwekewa Urusi ni wanariadha wake kutoshiriki katika michezo yoyote ya Olimpiki ama Paralympic huku mashindano ya Olimpiki yakitarajiwa kufanyika mjini Tokyo iwapo virsui vya corona vitazuiwa.
Vile vile Urusi ilikuwa imepigwa marufuku ya kuandaa michezo huku wanariadha wa taifa hilo ambalo hawana makosa yoyote ya kutumia dawa za kusisimua misuli wakiruhusiwa kushiriki katika mashindano mengine.
Uchunguzi wa WADA ulibaini kuwa maabara nchini Moscow ilitoa taarifa za uongo kuhusiana na vipimo vya wanariadha wa taiafa hilo kati ya mwaka 2012-2015 .