Hatimaye Inspekta Mwala afunguka baada ya tukio la kugonga na kuua Kaloleni

Image83828_1
Image83828_1
Baada ya muigizaji Davies Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala kuponea kichapo cha umati Kaloleni, mcheshi huyu sasa amefunguka kuhusu tukio nzima. Mwala alihusika katika ajali mbaya na kumgonga na kuua mpita njia papo kwa hapo katika barabara ya Kaloleni- Mazeras kaunti ya Kilifi.

Soma mengine:

Katika mtandao wa Twitter, Mwala ametuma pole kwa familia ya Samuel Mwaki.  Taarifa zinaonyesha kuwa Mwala alikuwa anasafiri kutoka hafla ya mazishi kuelekea Mombasa alipohusika katika ajali hii. Maafisa wa polisi walifika ghafla kumkinga na wananchi waliotaka kumvuruga baada ya kisa hicho.

Soma mengine:

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Patrick Okeri amesema kuwa Mwala alikuwa ameendesha gari aina ya Toyota Axio usiku wa jumatatu alipotatizika barabarani na kumgonga Samuel Mwaki.

“Sina la kusema. Polisi wanajua kilichofanyika,”Mwala alibana kueleza matukio alipopigiwa simu na gazeti la Star.

Mwili wa mwendazake ulikimbizwa Coast General Hospital huku gari ya Mwala ikisalia katika kituo cha Polisi cha Rabai.