Hatimaye Mkewe Ali Kiba afunguka mengi kuhusu talaka

taDk9kqTURBXy8zNWMxMWViMjQxZTdlMjE1ZmIxMGFhZjY5YjAzZTBjMy5qcGVnkpUDADXNAtrNAZuTBc0DFM0BvIGhMAE
taDk9kqTURBXy8zNWMxMWViMjQxZTdlMjE1ZmIxMGFhZjY5YjAzZTBjMy5qcGVnkpUDADXNAtrNAZuTBc0DFM0BvIGhMAE
Siku chache baada ya taarifa kuwa nyota wa Bongo Ali Kiba amemtema mke wake, Amina khalef ametokea kupinga taarifa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa za East Africa TV, Ali Kiba alifikia uamuzi wa kumpa talaka mkewe baada ya kushindwa kufikia suluhu mwafaka.

Taarifa ziliarifiwa kuwa maisha ya Ali ya nyuma yalichangia talaka hii.

Zaidi ya hapo wanawake ambao Kiba amezaa nao walizua kizungumkuti katika wanandoa hawa.

Soma hadithi nyingine:

“Msanii Ali Kiba amempa talaka tatu mkewe Amina Khalifa raia wa Kenya baada ya kushindwa kupata muafaka kuhusiana na ugomvi wao na ndugu wa Alikiba na Mama wa Alikiba… ,” Taarifa ya East Africa TV ilidokeza.

Mkewe sasa amekana taarifa hizo kupitia Insta.

https://www.instagram.com/p/B2pjmuRgUMO/

"Mimi mbona naishi nao Mashemeji zangu,,,nimewakuta nitaishi nao na bado tunakula wote kila siku😍😍😍😍." Alisema Khalef

"Ndoa yangu naipenda, pia nalinda maslahi yangu..nampenda mume wangu."

https://www.instagram.com/p/B2hMqe4Age0/

Soma hadithi nyingine:

"NDOA TAMU MUME ONGEA💍👑🤲🏻😍"

Katika mahojiano ya nyuma, Ali Kiba alikiri kuwa ndoa yake na Amina Khalef ipo katika wakati mgumu na kuwa inakumbwa na matatizo tele.

“Ni ukweli kuwa mimi na bibi yangu tuna matatizo, na hili ni jambo la kawaida kwa wanandoa…”

Soma hadithi nyingine:

“Nilimrudisha kwa wazazi wake Kenya. Nilitaka pia yeye afanye kazi halafu nikasafiri Uropa.”

” Hapo mwanzoni alikuwa amenitaarifu kuwa angependa kufanya kazi kwa sababu amesoma sana.

“Nilipotoka Uropa akaniambia yuko poa na nina ruksa ya kuenda kumwona kwao.”

“Sijampa talaka mwanzo ila kitu mtu anafanya ya kwake. Talaka sio kitu cha kusifia au ata cha kutangazia watu.”

Kiba alisema kuwa mamake alikuwa wa msaada sana kuwaleta pamoja.