Hatimaye Mzee Moi apata nafuu, aruhusiwa kuondoka hospitalini

Rais mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi hatimaye ameondoka kutoka Nairobi Hospital alikokuwa akitibiwa baada ya kupata nafuu.

Kikosi cha utabibu wake kinaongozwa na daktari David Silverstein aliidhinisha kuwa Mzee Moi yu nafuu kiasi cha kuruhusiwa kuondoka hospitalini

"Familia ya Moi inawashukuru wale wote waliomwombea na kumtakia nafuu ya haraka," katibu wa kibinfasi wa  Moi Lee Njiru alisema Alhamisi.

Moi alilazwa hospitalini Nairobi siku 10 zilizopita  katika kitengo cha hali mahututi, chini ya majuma mawili tu baada ya kutibiwa katika hospitali hiyo.

Madaktari wanasema kwamba mzee Moi mwenye umri wa miaka 95 alikimbizwa hospitalini kutoka makao yake ya Kabarnet Gardens iliyoko jijini Nairobi.

Mnamo Machi 2018, Moi alisafirishwa hadi Israel kutokana na kile "Maumivu katika goti lake."

Januari 27, 2017 alifanyiwa upasujai katika goti lake kwenye Aga Khan University Hospital jijini Nairobi.