Hatua kubwa alizozifanya Konde Boy baada ya kuitema Wasafi

68982464_381056136120833_6438164767961324750_n
68982464_381056136120833_6438164767961324750_n

Miezi imepita sasa tangu staa wa muziki nchini Tanzania aiteme lebo ya WCB.

Maendeleo na nyota katika kazi za staa huyu zinaonekana ziking'aa tofauti na wapinzani walivyodhania.

Harmonize ameweza kuoa Sarah mrembo mwitaliano na hakuwashirisha mastaa wenzake wa kundi la Wasafi.

Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize anazidi kung'ara hata zaidi.

Soma hadithi nyingine;

Konde Boy ameteuliwa kushindania tuzo ya mwanamuziki bora wa Afrika katika tuzo za muziki za MTV Ulaya.

Mastaa waliokuwa wanabishana levo moja ni Nasty C na Prince Kabyee, Toofan, na Burnaboy kutoka Naijeria.

" Mfalme Kijana wa Muziki Afrika Mashariki , #KondeBoy @harmonize_tz ameteuliwa kwa tuzo kitengo cha mwanamuziki bora wa Afrika 2019 MTV EUROPEAN MUSIC AWARDS," uliandikwa ujumbe wa MTV Africa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

https://www.instagram.com/p/B3KFkvunr9m/

Kupitia uteuzi huu, Harmonize anaweka rekodi ya staa wa kipekee kuteuliwa katika ukanda wa Afrika Mashasriki na kati.

KondeBoy akitwaa ushindi katika tuzo hizi atakwenda sawa na aliyekuwa bosi wake.

Soma hadithi nyingine;

Inaonekana kuwa nyota ya staa huyu inazidi kung'aa baada ya kutema lebo iliyomkuza.

Meneja mmoja wa WCB Sallam SK alitangaza kuwa staa huyu bado yupo WCB kimkataba.

"Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi,"