Hatua ya haraka! Kenya yaanza mchakato wa kupima madereva wa masafa marefu mipakani

NA NICKSON TOSI

Hatua ya visa ambapo madereva wa masafa marefu  kutoka taifa jirani la Tanzania kuendelea kugunduliwa na visa vya virusi vya Corona nchini Uganda na kuibua hisia kinzani jinsi uongozi wa John Pombe Magufuli unavyochukulia swala la Virusi hivyo, serikali ya Kenya hii leo sasa imeanza rasmi mchakato mzima wa kuanza kuwapima madereva hao wanaotoka katika mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

Katika mpaka wa Kenya na Uganda, mlolongo mkubwa wa malori hayo umeshuhudiwa huku maafisa wa afya wakilazimika kuwakagua madereva hao mmoja baada ya mwingine.

Kati ya visa 79 ambavyo taifa la Uganda limesajili kwa sasa, 22 kati ya hivyo visa vimetokana na madereva ambao wanasafiri kutoka taifa la Tanzania na Kenya .

Hatua ya kuwafanyia vipimo maderava hao imechukuliwa kwa haraka na serikali baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya madereva wa masafa marefu kutoka Tanzania ni waathiriwa wakuu.