Hatujamalizana na makamu wa chansela wa maasai Mara - DPP

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji amewashauri wananchi kupuuza uvumi ulioandikwa na mwananchi mmoja katika mtandao wa kijamii wa twitter akisema kuwa Mary Walingo ameachiliwa huru kwa mashtaka ya ufisadi yaliomkumba mwaka jana.

Makamu wa chansela Mary alikabiliwa na mashtaka ya kutumia fedha na mali ya chuo hicho vibaya.

Hakji kwa kupitia mtandao wa kijamii wa twitter aliandika kuwa mashtaka inazidi kuchunguza kesi hiyo, na wakimalizana nayo watafahamisha wananchi watakapo maliza uchunguzi wao.

Uvumi huo ulikuja baada ya mwananchi mmoja kuandika kuwa Mary Walingo hayumo tena mikononi mwa DPP.

Mwalimu Mutemi wa Kiama@MutemiWaKiama

UPDATE: Maasai Mara University Vice Chancellor Prof Mary Walingo reinstated after 4 months of state-led investigations that found no evidence of corruption allegations leveled against her.What does "DCI" stand for? Dry Cleaning Investigations? !

DPP alishauri watu waweze kutupilia mmbali uvumi huo kwa maana ni wa uongo, na uliandikwa ili kuvuruga uchunguzi wa kesi hiyo.

ODPP_KE@ODPP_KE

Contrary to allegations contained in post by , Maasai Mara University VC Prof. Mary Walingo has not been cleared of corruption allegations against her. File is still under review & once ready, DPP will direct appropriatly.

ODPP_KE@ODPP_KE
 

We urge the public to treat this information as false and malicious and aimed at interfering and diverting attention and undermining the work of investigative and prosecution agencies.

Makamu huyo wa Chansela aliweza kurekodi kauli  mwaka jana kufuatia mashtaka hayo.
Mary alichunguzwa na ofisi ya uchunguzi wa kigaidi mwaka jana na kueleza kwa undani jinsi millioni 190 ziliweza kutolewa katika akaunti ya chuo hicho bila kufuata mchakato.

Wanahabari waliweza kuandikisha kauli katika ofisi ya DCI na kueleza jinsi fedha na mali ya chuo hicho zilivyo tumiwa vibaya na wasimamizi hao.

Muungano wa wafanyikazi wa vuo vikuu kenya ulisema kuwa Mary hakuweza kufaulu na hakustahilii  kuwa katika ofisi hiyo.

Katibu mkuu wa Uasu Wasonga baada ya kesi hiyo kufichuliwa alisema kuwa Walingo anapaswa kutoka katika ofisi na kukubali uchunguzi ufanyike.
Pia katibu mkuu wa Kusu Charles Mukhwaya alisema profesa huyo anapaswa kutoka ofisini mpaka uchunguzi uweze kukamilika.