‘Hatukuibia mtu,’ mwelekezi wa Diamond na Tanasha akanusha madai

'Director' Kenny ndiye alisimamia kurekodiwa kwa video ya wimbo 'Gere' wa Diamond na Tanasha. Wimbo huo umetamba sana na mwanamziki raia wa Brazil Iza hakufurahishwa na kudai kwamba waliiba ubunifu wake wa video.

Video hizo mbili zinakaribiana sana katika mipangilio yake. Wimbo wa Iza 'Brisa' ulitolewa miezi kumi kabla Diamond na Tanasha kutoa wimbo wao 'Gere' na ambao ulipata ushabiki mkubwa katika mitandao na kutazamawa na mamilioni ya watu.

Iza kisha alizamia mitandao ya kijamii akilalamikia kuibwa kwa ubunifu wake wa video na inaonekana Diamond na Tanasha hawakuomba ruhusa kutumia ubunifu wa wenyewe. Kwa ufupi ni 'wizi wa mchana'.

Lakini akizungumza katika mahojiano kwenye wasafi TV, mwelekezi wa Diamond, Kenny alisema kwamba hakuiba ubunifu wa mtu yeyote na kwamba akili zimekuwepo na haziwezi kuwa eti zinamilikiwa na mtu mmoja pekee.

‘Hamna ubunifu wa mtu mmoja duniani. Haya mambo huwepo tu. Akili hizi zinaweza fanana na sio kwamba nimeiga, kama tungeiba si tungesafiri huko kwao tutumiye bichi zao, tutumiye kila kitu walichotumia katika video yao, huu ulikuwa ubunifu wangu. Niliunda seti nzima ya vide hiyo na mtu yuaja kuniambia kwamba niliiba? ni ubunifu tu’