Hatukujua alikuwa rubani wa William Ruto - Gladys Magonga asema

Familia ya mwendazake rubani wa naibu rais Mario Magonga aliyepata ajali ya ndege katika eneo la Turkana kisha kufariki waliweza kusema kuwa, alikuwa mwenye bidii na pia aliipenda kazi yake sana.

Rubani Mario aliweza kufariki Jumapili usiku na ndiye alikuwa tegemeo la familia hiyo ambayo ilishikwa na huzuni mwingi baada ya kupata habari kuwa Mario amefariki.

Wakati wa mahojiano na mama wa rubani huyo mwenye umri wa 45, Melania Magonga, aliambia KNA kuwa alisikia uchungu mwingi kwa kumpoteza mwanawe.

Mario alikuwa amehaidi mama yake kuwa atamjengea nyumba yake kwa shamba ambalo alikuwa amenunua eneo hilo la Kitale.

"Kabla ya habari hizo kunifikia asubuhi, nilikuwa nasikia moyo na mwili wangu ukiniambia kuna jambo mbaya, lakini sikua natarajia jambo la kifo." Alisema Melania.

Alisema mume wake Brigadier Magonga aliweza kuuwawa miaka 25 iliyopita na maisha kwake hayajakuwa rahisi tangu mume wake afariki.

Ndege hiyo inaripotiwa kuanguka katika eneo la (Cental Island National Park) Turkana saa mbili usiku huku ikiwauwa watu wote ambao walikuwa katika ndege hiyo.

Gladys Magonga ambaye ni dada yake rubani huyo alisema kuwa aliweza kupokea habari hizo saa kumi na moja asubuhi ambapo alipigiwa simu na mke wa ndugu yake ambaye anaishi nairobi na kumjulisha.

Gladys aliweza simulia nduguyake kama mtulivu na hakuweza kuhusisha mtu yeyote kwa kazi ambayo alikuwa anafanya.

"Nilishtuka sana nilipopata habari hizo, tuliweza kwanza kuficha mama yangu habari hizo kwa maana ana masuala ya afya. Habari hizo zilikuwa kila mahali, tuliweza kuzima runinga hata redio na kuzima simu ya mama yangu."Aliongea Gladys.

Kulingana na Gladys, familia haikuwa inajua kuwa ndege hiyo ilikuwa ya naibu rais kwani walijua baada ya ajali hiyo kutendeka.

"Nilijua tu alikuwa rubani lakini sikujua alikua rubani wa naibu rais William Ruto," Alisema.

Alimuomba naibu rais kuingilia kati na kumalizia mradi ambao alikuwa ameuanzisha na pia kuwalea watoto wake watatu.

Mabaki ya ndege hiyo na miili ya marehemu ziliweza kupatikana jumatatu asubuhi, watalii hao walikuwa wametoka kutembea Lobolo tented camp,na walikuwa wanarudi ndipo walipo patana na ajali hiyo.