Hatutaki vituo vya polisi Kibra, MacDonald Mariga

Vituo vya polisi katika eneo bunge la Kibra vitageuzwa vibanda iwapo Mariga atapata kiti hicho cha ubunge hapo kesho.

MacDonald amesema kuwa haoni maana yoyote ya vituo hivyo katika mtaa huo wa mabanda.

Staa huyu wa soka ametangaza haya huku masaa yakisalia ili uchaguzi ufanyike.

Hapo kesho tutashuhudia kinyanganyiro kikubwa kati ya wagombea wengi wanaomezea mate kiti hiki.

Farasi wanaonekana kuwa wawili, Imran wa ODM na Mariga wa Jubilee.

Kinara wa ODM Raila Odinga amewakaribisha magavana wa ukambani, Waiguru na viongozi wengine ili kumpigia debe Imran katika eneo.

ODM inapambana juu chini isipoteze ngome yao kwa Jubilee.

Kiti hiki kilisalia pengo kubwa baada ya ndugu yake Imran Ken Okoth kufariki.

"Hatutaki vituo vya polisi Kibra, tutapunguza idadi ya vituo na badala yake kubuni biashara ambayo itawakimu vijan akama duka ya kinyozi, kuosha gari na salon." alisema Mariga.

Aidha, Mariga ametoa taarifa za kuhalalisha matumizi ya bangi,

"Wacha tuzungumze kuhusu bangi, tunajua inatibu kansa, Tunatakiwa kuishinikiza. Hata hivyo, hatutaki itumike kwa njia mbaya. Nipigie kura na nitaishinikiza," alisema Mariga.