Hatutaweza kumwita nabii Owuor hivi karibuni - DCI

1904497
1904497
Wafanyakazi wawili wa nabii Owuor walifika jana katika kituo cha polisi cha Kabete ili kuandikisha taarifa. Wawili hao walikuwa wanaamini kuwa walikuwa wanamfanyia Jayne Muthoni kazi.

Hii ni baada ya mchunguzi wa DCI Francis Wanjau kusema kuwa hawataweza kumwita nabii Owuor hivi karibuni kuhusiana na madai kuwa alinyakuwa mali ya Jayne Muthoni.

Walikuwa pamoja na msimamizi wa kanisa Lily Macharia ambaye pia aliweza kurekodi kauli yake Jumatano katika kituo hicho.

Kulingana na Wanjau waliweza kuwaita wafanya kazi hao ili waweze kujua ukweli wa madai kuwa Muthoni aliweza kupotoshwa akili.

"Wafanya kazi hao wataweza kusema kama Muthoni alikuwa anakunywa dawa, kwa maana wamekuwa wakiishi na yeye."  Wanjau alisema.

Hata hivyo wanahabari waliweza kuzuiwa na polisi kuwaona wafanyakazi hao, huku wachunguzi wakikanusha madai kuwa Owuor ataweza kuenda katika kituo cha polisi kurekodi kauli yake.

" Nabii Owuor si mukorino wakutoka Kawangware kwa hivyo hatuwezi muita hivi hivi tu." Aliongea Wanjau.

Jumatano afisa mmoja wa DCI aliambia gazeti la The Star kuwa wameweza kumtumia Owuor barua ili kuchagua siku ya kurekodi kauli yake kati ya Alhamisi na Ijumaa.

Familia ya Muthoni wameweza kumshtaki nabii Owuor kwa kunyakua mali ya Muthoni aliokuwa nayo.

Aliongea zaidi na kusema kuwa Muthoni alipelekwa hospitali kwa matibabu na kuangaliwa kama yuko timamu, na bado hajaweza kurekodi kauli yake.

"Madaktari wanapaswa kuangalia hali yake ya akili kwa makini, na kisha watuambie matokeo yake, hii ni kwa sababu anaweza kurekodi kauli alafu mwishowe aseme kuwa hakuwa katika hali sawa au hakuwa timamu." AlielezaNjau.