Hawa hapa wanasiasa wa kike wenye mavazi na mitindo ya kupendeza .

Ni  wanawake thabiti  ,wana umahiri na  weledi wa kipekee  na wamejitosa katika siasa  na kuzipiga kama wazoefu . Pia urembo wao hauzui ubishi na mitindo yao pia  inatesa .

hii hapa orodha ya baadhi ya wanasiasa wa kike walio na mitindo ya mavazi ya kuvutia .

Esther Passaris( umri ,miaka 54)

Passaris ambaye  ni mfanyibiashara ,mhisani na mwanasiasa ni mrembo wa kuchachawiza . mavazi yake na miondoo pia haijanyima chochote na wakati wote akiwa  amejikwatua kuvutia . Pia amefahamu jinsi ya kila mara kuonekana chipukizi na kamwe umri haujamasaliti.

Anne Waiguru( Miaka 52)

Gavana huyu wa Kirinyaga  wakati wote anapendeza kwa ajili ya mavazi yake  bomba . Rangi nyekundu bila shaka ndio chaguo lake .

Susan Kihika( miaka 45 )

wakili huyu ambaye ni seneta wa nakuru  wakato wote anavutia kwa ajili  mkwatuo wake wa kupendeza . mtindo wake hauhitaji kumtoa jasho ili kuonekana kama ua .

Wavinya Ndeti( Miaka 51 )

mwanasiasa huyu  wakati wote  anabubujikwa usasa na anavutia katika muonekano . ni mojawapo ya wanasiasa wa kike wenye miondoko ya kisasa .

Millicent Omanga

Seneta huyo chipukizi ana  mvuto wa umbo ambalo wengi huzuzulika nalo- na amefahamu  makali ya umbo hilo hivyo basi mavazi yake huingiana vyema sana na mwili wake .

Sonia Birdi

mwanamke wa kwanza    mwenye asili ya kiasia kuhudumu katika bunge la taifa .  Urembo wake wa kiasili na bayana  na bila hajafelisha kupitia  mavazi na mtindo wake . wakati wote ana muondoko  ya hadhi  na wa kipekee .