Haya ni mapenzi kweli?Binti auawa baada ya kukataa kuchumbiwa

Kidosho mmoja kutoka nchini Tanzania jina lake Betha Kafura aliuawa na mpenzi wake baada ya kukataa kuchumbiwa na jamaa huyu.

Inasemekana jamaa huyu alikuwa amekasirika sana baada ya Betha kukataa kufunga ndoa naye kwani ni jamaa huyu aliyegharamia maisha ya Betha.

Jamaa huyu jina lake James Paulo mwenye umri wa miaka 27 alitiwa mbaroni baaada ya kumuua Betha.

James Paulo ambaye ni polisi wa Tanzania alimpiga risasi mpenzi wake kichwani na kumuua papo hapo.

Kisa hiki kilifanyika nyumbani kwa mshukiwa huyu Tunduru,Ruvana.

 Wenye mamlaka nchini Tanzania waliwaambia vyombo vya habari kuwa Paulo alimuua mpenzi wake baada ya kukataa kuolewa naye hata baada ya paulo kugharamia masomo yake Betha ya chuo kikuu.

Marehemu Betha kafuru alimaliza masomo yake ya Diploma ya uuguzi juzijuzi.

Paulo aliwaambia polisi kuwa alikuwa anatarajia kufunga ndoa za maisha na mpenzi wake Betha ambaye ni mama ya mtoto wake baada ya Betha kumaliza masomo yake kwenye chuo kikuu.

 Tazama orodha ya ujumbe wa rambirambi uliotolewa  na mashabiki wa Tanzania

''Mungu ametoa na mungu ametwaa pumzika kwa aman betha kafuru huu                     utawagusa wooote waliosoma mboza mission mbeya huyu alikuwa Mtoto wa              sekend master kafuru hakika mungu yu mwema pumzka kwa aman dogo weetu.''

Mwingine alisema,

‘PUMZIKA KWA AMANI MWENYEZI MUNGU AKUEPUSHE NA ADHABU YA KABURI AMINA’