Hayo ni Mapepo! Mwanamke aliyewaua watoto wake 4 alaumu mapepo kutoka kwa mpenziwe wa zamani

mapepo
mapepo
Mwanamke aliyekamatwa kwa kuwaua watoto wake wanne huko naivasha amesema aliongozwa kufanya hivyo na mapemo ya mpenzi wake wa zamani .

Beatrice Mwende, 42, amesema  alikuwa ameingilia na mapepo na yungali anafikiri yupo kwenye ndoto baada ya kutekeleza mauaji ya wanawe  na sasa anamlaumu mpenzi wake huyo waliyetangana naye mwaka jana . Mwende  amesema anapitia uchungu nab ado hajaelewa kilichofanyika .Alifikishwa kortini  jana mbele ya hakimu mkaazi wa Naivasha   Yusuf Baraza.

Mama huyo wa watoto sita  alisimulia jinsi walivyowauawa  watoto wake wanne siku ya ijumaa kwa kuwapa sumu kabla ya kwenda kulala .

Mwende,  mwalimu wa hesabu  aliyekuwa akifanya kazi na shirika moja lisilo la serikali mjini Naivasha  aliomba msamaha kwa hatua hiyo yake na kutaka ahurumiwe  akisema hakujua alikuwa akifanya . “ Mpenzi wangu wa zamani alikuwa na nguvu za mapepo alizotumia kunielekeza kufanya unyama huo  na kusababisha niwaue watoto wangu wanne’ alisema

“ Nataraji kwamba ndoto hii mbaya itakamilika na nitaamka niipate familia yangu katika nuzri ya afya kwa sababu siwezo hata kumdhuru nzi’

Watoto waliouawa wametambuliwa kama  Melody Warigia (8), Willy Macharia (6) —  wote wanafunzi wa shule ya  Milimani Primary School, Samantha Njeri (4)  na Whitney Nyambura (two).

Polisi huko Naivasha wameruhusiwa kumzuilia Mwende kwa siku saba  ili kukamilisha uchunguzi wao .

Mshukiwa atafikishwa tena kortini Julai tarehe 6 .

Polisi watategemea ripoti ya uchunguzi wa miili ya watoto hao na ripoti wa hali yake ya kiakili .Akikumbuka uhusiano wake wan a mpenzi wake ,Mwende amedai kwamba alikuwa na nguvu za kumfanya atekeleze mambo ambayo hakutaka .

Amesema kwamba  tarehe  26 ya kila mwezi  alikuwa akiingiliwa na mapepo yaliyomfanya  kufanya vitu  bila kuweza kujithibiti . Alimtaka mungu na familia yake kumsamehe kwa mauaji aliotekeleza ya wanawe .

Mwende  amesema jumamosi asubuhi baada ya kugundua alichofanya alienda naivasha kumtafuta mwanamme huyo ambaye hufanya kazi mjini Naivasha . Kupitia barua alioandika Mwende  amesema alishangazwa na hatua hiyo yake na kwamba alikuwa tayari kwenda jela kwa makosa aliofanya .