Ndungu wa chanda na pete

HEAD TO HEAD:Ruto amtia makucha Kenyatta wazi wazi-GLOVES ARE OFF!

Naibu wa rais William Ruto amechoka kuwa mustaarabu  na sasa amepata ukakamabvu wa kumkosoa hadarani rais Uhuru Kenyatta hasa kuhusiana na   ripoti ya BBI na siasa za  uchaguzi wa mwaka wa 2022 . Ruto amesema rais Kenyatta na Kiongozi wa ODM Raila Odinga wanafaa kuwaeleza wakenya bayana nia yao na  ripoti ya BBI baada ya kenyatta kuweka katika gazeti rasmi la  serikali   arifa ya kuwaongeza muda wanachama wa jopo kazi la BBI .

SAD:Mvulana mwenye umri wa miaka 11 amuua kakake wakipigania chaja ya simu

Arifa hiyo ya gazeti rasmi la serikali  sasa inatoa fursa kwa jopo hilo la wanachama 14 kuifanyia marekebisho ripoti ya mwanzo iliyokuwa imetolewa kwa umma . Washirika wa Ruto hata hivyo wanashuku kwamba rais  na Bwana Odinga wana hila dhidi ya Ruto na wanalenga kuitumia ripoti hiyo a BBI kumzuia naibu wa rais Kumrithi rais Kenyatta baada ya uchaguzi wa 2022 .

Matiang’i for PM:Maina Kamanda asema watamwunga mkono Matiangi kuwa waziri mkuu

Wanachama  wa jopo kazi hilo ni seneta wa  Garissa Yusuf Haji, Askofu Lawi Imathiu, Maison Leshomo, James Matundura, Rose Museu, Agnes Kavindu and Saeed Mwaguni. Wengine ni Askofu Peter Njenga askofu mkuu  Zaccheaus Okoth, Adams Oloo, Seneta  Amos Wako, Florence Omose, Morompi Ronkei  na John Seii. Makatibu wa pamoja wa jopo hilo ni Martin Kimani  na  Paul Mwangi.  Kamati hiyo itawakabidhi rais na bwana Odinga ripoti yake  Kufikia Juni tarehe 30.

 

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments