‘Hebu nione ball yangu,’ Eric Omondi amuomba Jacque Maribe

24354f
24354f
Siku chache zimepita baada ya aliyekuwa mpenzi wa Jacque Maribe Dennis Itumbi kuupuzilia mbali ujauzito wake, sasa mcheshi Eric Omondi katika mtandao wa kijamii wa insta amechapisha video akimuomba Maribe ruksa aweze kuuona ujauzito wake.

Soma hadithi nyingine:

Ubuyu upo kitaani kuwa wawili hawa waliwahi kuwa na uhusiano wa karibu zaidi katika nyakati za hapo nyuma. Katika chapisho hilo lililochapishwa katika mtandao wa kijamii wa insta na kufutwa ghafla. Eric anasikika akisema.

"Niko hapa nawatch ball yangu. Harambee Stars wametuangusha. So wacha niwatch ball yangu. Kila mtu awatch ball yake." alijinadi staa huyu.

Kama utani, Eric anamwambia Jacque amruhusu aone ujauzito wake.

"Hebu nione ball yangu." Omondi alimwambia Maribe.

Soma hapa:

Jacque anamcheka sana Omondi na kumwambia amuondokee. Katika mahojiano ya hapo awali na kituo cha Radio Jambo, mtaalam huyu wa ucheshi aliwahi kufunguka jinsi walivyofahamiana na binti huyu.

"Nilimpata Jacque kitambo tukifanya kazi Radio Africa Media Group na urafiki wetu ukakua kutoka pale. Tuliwahi ata kwenda Sarit tukakunywa chai. Tangia hiyo siku urafiki wetu ukawa imara." Eric Omondi.