Hela yatolewa kufadhili mazishi ya Mariam Kighenda na Amanda, KFS yatoa pole

G7i9HLd7cUt1HbWik__1571145231_40004
G7i9HLd7cUt1HbWik__1571145231_40004
Shirika la feri nchini limetoa taarifa kuwa imeikabidhi familia ya marehemu Mariam Kighenda na Amanda Mutheu shilingi  200,000 ili kusaidia familia yake kwa mazishi.

John Wambua pia amepokea 682,500 kutoka kwa kampuni ya bima ya gari lake

Shirika hili limetoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter.

Haya yanajiri baada ya mmewe John Wambua kukana taarifa za huenda mkewe alijiua kupitia mkasa huo.

Katika mahojiano na kituo cha runinga cha NTV, mmewe Mariam John Wambua alitetea mkewe kuwa hakuna uwezekano wowote wa kurudisha gari nyuma na kutumbukia baharini.

"Hii leo serikali (KFS) imeikabidhi familia ya marehemu Mariam Kighenda na mtoto wake Amanda Mutheu shilingi 200,000...." KFS ilichapisha katika Twitter.

Wambua alikuwa akikana taarifa kuwa huenda mkewe alikuwa na njama ya kujiua pamoja na mtoto wake.

 Bwanake alisema kuwa gari la mkewe lilikuwa katika hali ya kuegeshwa huku akiwasihi wanapolisi kuharakisha zoezi la uchunguzi.

Haya yanajiri huku feri zilizopo katika kivukio hicho zikidaiwa kuwa mzee zaidi na zina zaidi ya miaka 30.

Kwa umbali, mabati ya feri hizo yana kutu kuashiria uzee.

Milango ya feri hizo na sehemu za kukanyagia unapoingia zimezeeka zaidi.

Wengi wanahoji kuwa hali mbovu ya feri pamoja na utepetevu kazini zilichangia pakubwa na kuwa ajali hii ingeepukika.

Aidha, nyufa za mamlaka ya feri nchini kukosa kuajiri wapiga mbizi ili waweze kusaidia kunapotokea ajali zimeonekana wazi.

Miili ya Mariam Kigenda na mwanawe wa miaka minne Amanda ilipatikana ikiwa imekumbatiana katika kiti cha nyuma ndani mwa gari lao.

Kisa hicho bado kinachunguzwa kwa kina ili kubaini kilichojiri.