NA NICKSON TOSI
Msanii wa nyimbo za kufoka almaarufu kama R$B Juma Jux kutoka Tanzania ameanza kumezea mate mfanyabiashara maarufu kutoka humu nchini Huddah Monroe kwa kile amekiri kuwa mwanamke huyo ako na umbo zuri la kuvutia wengi.
Aidha usemi huo wa Jux huenda ulisababishwa na hatua ya Huddah kutuma picha zake kwenye mitandao ya kijamii akiwa nusu uchi na zikionyesha baada ya sehemu zikiwa nusu uchi.
Baada ya kupiga picha hizo Monroer aliandika hivi
"Rangi ya manjano inayozunguka kiza ambacho kimezunguka ulimwengu. 🥰".''aliandika Huddah
Juma ambaye kwa kuona tu ujumbe huo alifuatisha ujumbe wake na kuandika hivi.
Asanti kwa kutuchangamsha macho rafiki 😂"aliandika Jux
Huddah naye akamjibu bila ya kupoteza muda kwa kuandika hivi ,asanti sana rafiki , nimekumiss kweli na kweli Zanzibar ndio mahali pazuri pa kuwa.aliandika Huddah".
Siku chache zilizopita Monroe alitakiwa kuelezea uhusiano wake na Jux hasa baada ya kuposti katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja katika viziwa vya Zanzibar .
Jumbe walikuwa wakiandikiana wawili hao mitandaoni ndizo hizi hapa.
Si mara ya kwanza kwa Jux na Huddah kudaiwa kuwa wapenzi kwani siku nyingi wamekuwa wakionekana pamoja wakijivinjari licha ya Jux na mpenziwe Niyaka wa miaka kuwa katika mishe mishe za kila mara.