strong woman

Heri Nife? Dadangu zangu wadogo wameolewa kabla ya mimi,maisha yamekuwa magumu!

Enzi hii ambapo kila mtu ana uhuru wa kuamua anachotaka na wakati anapokitaka ina mkinzano mkubwa sana kuhusu jambo moja .

Shock!Siku niliyotakiwa ‘kulala’na maiti ya mume wangu kabla hajazikwa

Ikifika kwa upande wa kina dada kupata mchumba na kasha kuolewa sio wote walio na bahati ya kufanikiwa kwa urahisi kwa sababu ya mambo mengi .Kwanza ,karne hii imewapa wanawake mwamko mkubwa na hawawezi kufanya jambo ili kuifurahisha jamii –lakini jamii imesalia kuwa na ukatili sana kwa wale amao wamebandikwa sifa za kutimu umri wa kuolewa ilhali hawajaondoka kwa wazazi wao. Ndio  jambo linalompa mawazo chungu nzima Grace Kadzo. Dadake zake wadogo wawili tayari wameolewa na  kata nzima ya Chodari huko kilifu haimpi usingizi  -kuanzia kwa shangazi  ,wajomba ,wifi  zake na kila anayemjua anamuuliza mbona hajaolewa ilhali wadodo zake washapata maboma na hata ku[ata watoto .

Mwanamme Kamili? Jamaa akiri kuwa na bibi WATATU huku wawili kati yao wakilala pamoja naye katika kitanda kimoja!

Kadzo amesomea ualimu na muda mwingi amekuwa Mombasa ,usasa umemfanya kujijua na kufahamu kwamba ana haki zake kwa mwanamke kwa hivyo hana mbio za kumkimbilia yeyote ili tu aonekana  keshakuwa mke wa mtu . Anataka mtu ambaye ataijua thamani yake ,kisomo chake na umuhimu wake lakini jamaa zake hayo hawayatambui! Wanataka aolewe na aolewe sasa ! Ila licha ya ujasiri wake  Kadzo ameanza kupatwa na mawazo tangia mwaka huu uanze. Umri wake haujasimama na sasa ametimia miaka 36.Uchumba aliofanya na wanaume kama wawili huko Mombasa haujafanikiwa kuwa uhusiano wa ndoa na sasa ameanza kujitiliadoa mwenyewe akihisi kwamba labda ana kasoro . Kinachompa hamaki na hata zaidi ni kwamba jamaa zake wengi wanafikiri kwamba hajui kujizungumzia na sasa wamekuwa kama mawakala wa kumletea wanaume  na wanasukumiza sana kwanza wazi wazi sasa yamfanya aonekana kama ‘ng’ombe’ wa kuuzwa .

‘HIVI MIMI SINA TATIZO NA MTU KUNILETEA MCHUMBA ,ILA SASA WAMEIFANYA IMEKUWA  KANA KWAMBA MIMI NI MAZIWA AMBAYO YANAHARIBIKA! KILA MTU ANALETA MTU NA YUATAKA NIANZA NAYE MAISHA HARAKA..NIMECHOKA SASA!’ amefoka Kadzo .

Kiafrika kutoolewa kwa mwanamke anapotimu umri  fulani ilikuwa skendo kubwa.Ungefanyiwa kila kitu ili uondoke uwaachie wenzio wadogo nafasi za kuolewa kwa sababu baadhi ya mila hazikukubali wadogo zako kuolewa kabla ya msichana mkubwa kupata nyumba .Siku hizo hata hivyo mila hiyo imewekwa kando kidogo na wasichana waliozaliwa nyuma wanawatangulia wakubwa zao kuolewa . Kadzo  anasema hataki kuolewa ila yuataka mume bora na sio bora mume .

‘MWANAMME ATAKUJA AKUCHUMBIE ,KASHA BAADAYE UNAGUNDUA NI BWEGE TU,MTU HANA KAZI,HANA MAAZIMIO WALA HATA KIPATO,ATAKUTUNZAJE HUYO?’ anauliza Kadzo .

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Kadzo anasema  jamii inafaa kuanza kuwavumilia wanawake wa umri wa juu ambao wamechelewa kuolewa kwa sababu hilo halimaanishi kwamba ni wanawake wenye udhaifu  wa aina fulani . Pia amewashuru wenzake ambao hawajafanikiwa kupata waume wasikate tama na wajiamini .  Anasema ulimwengu wa sasa umebadilika na ndoa haifai kuchukuliwa kama mojawapo ya mafanikio ya mtu katika maisha .

‘ILI MRADI MCHANGO WAKO KWA JAMII NI MZURI ,SIONI IWAPO NI BORA NDOA KUTUMIWA KAMA KIGEZO CHA KUAMUA  ALIYEFAULU MAISHANI HASA KWA WANAWAKE’  anatamatisha Kadzo .

Kadzo anawazungumzia wengi walio katika hali kama yake . Ole wako iwapo wewe ni mwamake wa kisasa ,huru na msomi au na pesa zako .Basi kila sababu  yako kukosa kuolewa itakuwa mambo yote hayo! Ah ,anaringa kwa sababu ya kazi ,masomo yake au pesa zake.Mazito kweli .

 

Photo Credits: Internet

Read More:

Comments

comments