‘ Heri Uniite mpango wa kando lakini sitaki kuwa bibi ya mtu’ Njoki

pjimage (1)
pjimage (1)
Njoki Kaberu* hana soni kusema kuhusu mtindo wa maisha yake ambao umemfanya kupitia mengi .Kutoka majeraha na alama za  mwili ambazo zinadhihirisha vita vyake vingi na wake za watu ambao humpoata na waume zao hadi  kuhama kutoka mmoja hadi mwingine baada ya ‘kuchoma  Picha’ katika mita aliotoka kwa sababu ya mazoea yake ya kuwatongoza na kuanza kuishi na waume za watu .Huyu amayeoana yote nab ado hakomi .

Njoki anasema hapedi kuwa katika uhusiano na wanaume wa rika lake aama ambao hawana wake . anasema mume mtu hakupi  matatizo mengi kwa sababu anakupa unachotaka nawe unampa  atakachao na maisha yanaendelea . Anasema  hataki kuolewa kwa sababu kulingana naye ,wanaume hawaridhiki na anaogopa kwamba  mume wake pia atamfanya kama wanavyofanya wanaume wa watu kwa kuwa na wapenzi wa pembeni .

Njoki anasema katika maisha yake yote mahusiano yake yamekuwa tu na watu walio na wanawake na anapenda hali iwe hivyo ili asijipate kautoa moyo wake wote kwa mwanamme mmoja ili tu baadaye aje kuffadhaishwa ama kuachwa . Amepigana na makumi ya wanawake ambao walimpata na waume zao mara si haba na hata amelazimika kubadilisha nambari zake za simu baada ya  baadhi ya wanawake ambao alikuwa akitoka na waume zao kuanza kumsaka kama mhalifu sugu .

‘Unapata bwana ya mtu anakutaka , na yuko na pesa ,wewe ni kumuambia unataka kuishi wapi na kila kitu anakupa’ anasema Njoki .

Anaongeza kwamba kuna watu wanaotazama mtindo wake wa maisha kama ukahaba lakini anapinga hilo kwani anasema kamwe hajawahi kuwa na zaidi ya mume mmoja wa mtu kwa wakati mmoja na yeye huingia tu katika uhusiano mume wa mtu baada ya kuachana na mwingine .

‘ Mimi si player na siwezi taka kujihatarisha kwa kuwa na wanaume wawili au watatu at the same time .So mimi huhakikisha kwamba nadeal na mtu mmoja-imagine mtu akikulipia keja alafu agundue kuna mwanamme mwingine huja kwa hiyo nyumba ….siwezi taka shida kama hiyo …’ anasema Njoki

Hadi kufikia sasa anasema amewahi kuishi na zaidi ya wanaume watano ambao walikuwa na  wake na familia zao .Anasema wakati uhusiano wake na mwanamme unapokwisha kwa sababu moja au nyingine yeye huhama mtaa huo na kumtafuta mwingine wa ‘kumueka’.

‘Life ya ndoa ni ngumu ndio  kwa sababu mimi hupendeleo huu mtindo wa kuwekwa, heri unite mpango wa kando lakini usiniite bibi yako’ Njoki anatamatisha