Heshimu Wanawake, Ruth Odinga Awashauri Wakuu Wa Chama Cha ODM

Naibu wa gavana kaunti ya Kisumu Ruth Adhiambo Odinga, amewataka wakuu wa chama cha ODM kuwaheshimu wanawake wanaolenga kuwania viti vya uongozi kwa tiketi ya chama hicho.

Kiongozi huyo amemtetea seneta mteule Elizabeth Ongoro, ambaye amesema hatakubali kuhujumiwa kwenye chama hicho.

Ongoro analalamikia hatua ya uongozi wa chama hicho, kumkabidhi mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang tiketi ya moja kwa moja kutetea wadhifa huo, licha ya seneta huyo kuonyesha nia ya kuwania ubunge wa Ruaraka kwa tiketi ya chama cha ODM.

Kwenye taarifa, Ruth Odinga amesema Ongoro ana haki ya kuwania nafasi anayotaka, akisisitiza kuwa anafaa kupewa fursa ya kuwania ubunge wa Ruaraka kwa tiketi ya chama cha ODM.

Haya yanajiri huku, Ongoro akishikilia kuwa atawania ubunge wa Ruaraka kivyovyote vile, akiapa kusalia kwenye Muungano wa National Super Alliance – NASA.