Hii hapa sababu ya msanii Alikiba kulazimika kuharisha tamasha yake ya nyumbani

Msanii wa Tanzani Ali Saleh Kiba almaarufu Alikiba amelazimika kuhahirisha tamasha yakeya kurudi nyumbani Kigoma, ni tamasha ambayo ingefanyika mnamo tarehe 31, Julai mwaka huu hii ni baada ya kifo chake rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Tamasha hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, imeharishwa hadi tarehe 14 Agosti mwaka huu, hii ni kuwapa watanzania fursa ya kumuomboleza rais mstaafu Mkapa.

“Habari ndugu zangu Watanzania, kama wengi mlivyosikia, taifa letu tumepata msiba wa Baba na Mlezi, Mzee Benjamin Mkapa aliekuwa rais wa awamu ya tatu, ni msiba ambao nimeupokea kwa masikitiko, imenifikia ghafla sana, lakini ni mapenzi ya Mungu. Naomba Mungu ampumzishe mahali pema

Kutokana na msiba huu mzito nimeahirisha show yetu ya KIGOMA iliyokuwa ifanyike tarehe 31 ili kushiriki katika msiba huu wa kitaifa mpaka tarehe 14 August 2020. Pia nimehairisha zoezi la upokeaji wa michango mbalimbali ambalo nilipanga kulifanya kesho katika ofisi za Clouds Media Mikocheni. Taarifa za siku ya kupokea michango kwa ajili ya kuweka kwenye - nitatangaza baada ya msiba kumalizika. Asanteni, natoa pole kwa watanzania na wapambanaji wote walioguswa na msiba huu ." Alikiba Aliandika.

Alikiba alikuwa ameandaa tamasha ya kurudi nyumbani baada ya miaka sita.

“Baada ya miaka 6, hatimaye tarehe 31 July 2020, Narejea Nyumbani KIGOMA!

Ndugu zangu wa KASULU, Buhigwe, Kakonko, Kibondo, Uvinza na maeneo yote ya KTown - shughuli yetu tutufanyia pale LAKE TANGANYIKA STADIUM 🏟 ”