Hii Wizara ya afya imejaa wezi wengi sana. Tutawafichua hivi karibuni - Mutahi

Baada ya shutuma kuzidi kutolewa kwa serikali kuelezea namma bilion za pesa zilivyotumiwa katika mchakato wa kukabiliana na virusi vya corona kutoka kwa wananchi, waziri wa afya sasa amesema kuwa hivi karibuni atafichua baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiiba pesa za umma.

Mutahi alisema hayo wakati ambapo alipokuwa anatoa taarifa ya kila siku kwa taifa na kusema baadhi ya wafanyakazi hao ni mfano mbaya kwa taifa .

Aliongezea kuwa baadhi ya maafisa hao walikuwa wanajaribu kufanya biashara na vifaa vya kuwakinga wahudumu wa afya almaarufu kama PPEs .

Hivi maajuzi, Mutahi aliwahamisha baadhi ya mafisa 30 kutoka kwa wizara hiyo ya afya katika mabadiliko ambayo yalitazamiwa kama njia ya kuwaondoa watu fisadi .

Amesema wajasusi kutoka idara ya DCI sasa wameanzisha mchakato wa kuchunguza baadhi ya maafisa katika wizara hiyo na wale watakaopatikana na makosa watachukuliwa hatua.

“This building has got its fair share of criminals. Like any other marketplace, there are a few mad cases in here. And we will unearth them. As we move on, we will unearth them,” amesema Mutahi.

Wife material! Arejelea kilimo baada ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya Jubilee

Ameongeza kuwa kuna baadhi  ya maafisa hao ambao walikuwa wanajiingiza katika biashara feki na kutoa zabuni ama tender na kampuni zingine ikihusisha wizara hiyo ya afya.

“These are public officers who will call a businessman and tell them that they have got an order which they can help get him with a fake tender; and that fake tender might even have a Ministry of Health logo because some criminal in here has given it out.”  Mutahi alielezea.

Kwa upande mwingine, Mutahi aliwashukuru maafisa wote katika wizara hiyo ya afya ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kila kitu kinafanyika katika njia inayofaa haswa wakati huu ambapo taifa linakabiliana na virusi hatari vya corona.