HIJACKED:Duale asema Wanasiasa wameuteka nyara mchakato wa BBI .

Duale
Duale
  Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale amesema  mikutano ya sasa ya ushauriano kuhusu  BBI imetekwa nyara na wanasiasa . Mbunge  huyo wa Garissa Township  amesema ni jambo la kufadhaisha kwamba  mchakato uliokuwa na nia njema sasa umetwaliwa na wanasiasa ili kuendeleza maslahi yao . mbunge huyo ametaja mikutano inayofanywa ya BBI katika sehemu mbali mbali za taifa kama ‘inayokanganya’.

“  BBI iliyoanzishwa na rais Kenyatta ilifaa kuwahusisha wakenya wote . ni jambo la kusikitisha kwamba sasa wanasiasa wameutakanyara utaratibu mzima na kusababisha mgawanyiko hata zaidi’ Duale amesema .Duale, ambaye hajahudhuria mkutano wowote wa BBI  ameshikilia kwamba hana mpango wa kuhudhuria mkutano wowote wa BBI  isipokuwa inayohudhuriwa na naibu wa rais William Ruto na rais Uhuru Kenyatta.

“ kwa sasa nimejawa na majukumu  ya bunge linalorejelea vikao vyake wiki ijayo .watu wa kaskazini mashariki mwa nchi wana matatizo mengi  kama vile ukosefu wa usalama ,kufungwa kwa shule na  suala la sensa .Haya ndio masuala ninayoyazingatia kwa sasa ‘ amesema Duale . Matamshi ya Duale yanajiri siku moja  siku mbili tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kusema  kwamba mikutano ya BBI inayoendelea katika sehemu mbali mbali za nchi hailengi kumtenga yeyote .