Wengi wanajua kwamba Diamond alimkabidhi Tanasha Donna zawadi ya gari aina hiyo wakati wa birthday yake . Yaonekana Mbosso amelirithi gari la Tanasha baada ya kuibuka uvumi kwamba mamake Diamond pia alikuwa amelichukua gari hilo. Kupitia mahojiano na Wasafi Media, Mbosso alisema
Niliambiwa nisipokuwa makini nitaambiwa kwamba gari hili langu ni la Tanasha. Hili ndilo gari langu ambalo nimekuwa nalo tangia mwaka uanze
Msanii huyo wa wimbo ‘Hodari’ kisha alionyesha risiti za kununua gari lenyewe.
Tanasha kwa upande wake amesema hana wasiwasi kuhusu anayemiliki gari hilo kwani ana magari mengi katika garaji yake. Alisema ;
The car is in Tanzania. I had no interest in taking it. I have my car here. I have my BMW actually its in the garage. I can get myself a car and what I need,that’s all that matters