Hivi karibuni dawa za kuzuia ujauzito zitauzwa dukani kama kondomu

contraceptives
contraceptives

Wanawake na wasichana wanastahili kupataka dawa za kuzuia ujauzito bila ya ushauri kutoka kwenye maduka maalum ya dawa na kuuzwa duka lolote tu, asema mtaalam wa afya ya uzazi.

Ripoti iliyotolewa na chuo cha madaktari bingwa wa afya ya uzazi cha Royal College nchini Uingereza kimependekeza kidonge kinachomezwa kama hatua ya dharura ya kuzuia mimba baada ya kushiriki tendo la ndoa bila ya kinga kuuzwa madukani kama kondomu.

Kuna masharti mengi sana linapokuja suala la kupata huduma za afya ya uzazi kwa wanawake nchini Uingereza, Ripoti hiyo imesema.

Na mahitaji yao yanastahili kupewa kipaumbele.

Ripoti hiyo kwa jina maslahi bora kwa wanawake, inatoa wito kwa wanawake kuruhusiwa kuchukua dawa ya kwanza ya kuzuia mimba wakiwa majumbani, pamoja na ile ya pili, iwapo watakuwa na uhakika kwamba ujauzito ni wa chini ya wiki 10.

Ripoti hiyo mpya ya chuo cha madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi ijuliakanayo kwa kifupi kama RCOG, inasema wanawake wanapaswa kuwa na uwezo wa kupata ushauri wa daktari wanapotaka miamba ama kwa njia ya simu au kupitia Skype.

Ripoti hiyo pia inapendekeza uwepo wa mtandao wa kliniki za afya ya wanawake zinazotoa huduma zote katika eneo moja kama vile uchunguzi wa ugonjwa wa saratani, upangaji wa uzazi na utoaji ushauri.

Kwa sasa, wanawake na wasichana wanahitajika kupata ushauri kutoka kwa mwanafamasia kabla ya kupata dawa za dharura za upangaji uzazi, ambazo zinatakikana kutumiwa ndani ya siku tano baada ya kushiriki ngono bila kinga.

Jambo ambalo linaweza kufanya"wasiwe huru, wahisi aibu ama kuhukumiwa", ripoti hiyo inasema.

Wanapendekeza kwamba dawa za dharurua za uzuiaji wa mimba, vipimo vya uja uzito na kondomu zipatikane katika maduka ya kawaida tu.

'Nilihisi kusalitiwa nilipojaribu kupata tembe za kuzuia mimba'

Jane mwenye umri wa miaka 25, kutoka West Midlands, alifukuzwa na mwanafamasia wa kwanza baada ya kutaka apewe dawa za kuzuia mimba kwasababu hakuwa na miadi na siku hiyo.

Baada ya kuzua vurugu, aliruhusiwa kuonana na mwanafamisia huyo na hatimaye akapata dawa alizohitaji lakini hilo lilifanikiwa baada ya maswali mengi.

-BBC