Hivi sasa! Maafisa wa polisi wavamia makanisa mawili ya katoliki Bungoma

NA NICKSON TOSI

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Bungoma asubuhi hii wamevamia makanisa mawili ya katoliki eneo hilo ambayo yamekuwa yakiendesha misa za kanisa kila asubuhi pasi ya kufuata amri ya serikali yakufungwa kwa shuguli zote za makanisa nchini kutokana na mkurupuko wa Corona.

Kwa mujibu wa agizo la rais Uhuru Kenyatta,hatua ya kuzitisha shughuli za makanisa nchini ilichukuliwa ili kupunguza idadi ya watu wanaofumukana kwa wingi katika eneo moja.