'Hakuna Mkenya anapaswa kufariki kwa ajili ya corona,' Mike Sonko asema huku akidai amepata dawa ya kutibu corona

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amesema hakuna mkenya yeyote anapaswa kuaga dinuia kwa ajili ya virusi vya corona,pia alitangaza yuko na mpango wa kuzindua vituo zaidi za kuwatibu wakenya watakao patikana na virusi hivyo.

Kupitia kwenye ukurara wake wa mitandao ya facebook alisema kuwa vituo hivyo vitakua na dawa ya kutib virusi hivyo.

Sonko alidai kuwa kuna binamu wake ambaye ni mfanyakazi wa bandari ya Mombasa alipatikana na virusi vya covid- 19 na alipona baada ya kutumia dawa ziitwazo hydroxychloroquine.

https://twitter.com/MikeSonko/status/1288017502073757697

Kulingana na Sonko,dawa hizo ndizo tiba ya virusi vya corona na zinapaswa kuidhinishwa na wizara ya afya na shirika la afya duniani, WHO.

" Wakenya hawafai kupoteza maisha yao kutokana na COVID-19, nimejaribu kupata tiba ya virusi hivyo, kuna binamu wangu ambaye anafanya kazi katika bandari ya Mombasa aliambukizwa virusi hivyo na alipona baada ya kutumia dawa za hydroxychloroquine."