Hofu kwa taifa! Hospitali ya Mbagathi na Kenyatta zimeanza kujaa wagonjwa wa Corona- Kagwe

mbagathi
mbagathi
Serikali sasa imesema kuwa vituo vikuu vya kitaifa ambavyo vimekuwa vikitumika kutoa matibabu kwa waathiriwa wa virusi vya corona  vimeanza kujaa kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa ambao wamelazwa katika vituo hivyo.

Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, kituo cha hospitali ya Kenyatta na Mbagathi vyote vimeanza kufurika na wagonjwa wa virusi hivyo huku idadi ya maambukizi ikiendelea kurekodiwa kila uchao.

Hospitali ya Mbagathi ina vitanda 112 huku hospitali kuu ya kitifa ya Kenyatta ikiwa na vitanda 456 ambapo kufikia Juni 3 ilikuwa imewachukuwa wagonjwa 346 walioambukizwa virusi hivyo.

Alhamisi akitoa takwimu za kila mara zinazohusiana na virusi hivyo nchini, Kagwe alisema kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa maambukizi hayo nchini hali yao ni nzuri na hivyo wanaweza kutibiwa nyumbani.

“If this is implemented it would free our health facilities from congestion because we are reaching, for example in Nairobi, at a time when both Mbagathi and Kenyatta University Hospitals are getting to full status,” Kagwe alisema.

Alisema kuwa wizara imeweka tayari mikakati ya kuanza kutoa mafunzo kwa jamii jinsi ya kushughulikia wagonjwa hao.

 “What this means is that  a lot of people in isolation facilities may be released to be taken care of at their homes. Provided two things happen; first that it is in line with new World Health Organization protocols we are still looking at and trying to customize and domesticate to our situation and secondly it has to do with facilities that families may have and where families are not able to self isolate/quarantine the government will still assist in the process,”alisema Kagwe.

Wakati uo huo Kagwe amewataka wananchi kujiepusha na unyanyapaa miongoni mwa watu wanaopona kutokana na virusi hivyo akisema ni sharti watu wazingatia masharti mapya yatakayowekwa na wizara kama njia ya kakabiliana na virusi hivyo.

“A time is coming when we cannot continue as usual and we have to change tack. When see people come home lets understand they are no danger to us and therefore there is no need for stigmatization. You will be safe but the people concerned will have to take care of them because they do not need hospitalization,”Aliongezea Mutahi.

Matamshi yake yaliungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa afya Dr Patrick Amoth aliyesema hakuna la maana kuwa na waathiriwa wa virusi hivyo hospitalini kujaza nafasi ilhali hali yao ya afya inaweza kudhibitiwa wakiwa nyumbani.

“This is a key intervention that is approved by the World Health Organization and it is meant to decongest health facilities and prevent the healthcare system from being overwhelmed,”“It makes no business sense to b able to manage these people in a hospital facility.” alisema Amoth