Hofu Murang'a huku mwili wa mwathiriwa wa virusi vya corona ukizikwa usiku

Hatua ya kuzika mwathiriwa wa virusi vya corona usiku kaunti ya Murang'a imeibua hisia mseto miongoni mwa wananchi huku visa vya maambukizi katika jimbo hilo vikiendelea kuripotiwa .

Baada ya mwili wa mwendazake kuondolewa katika hifadhi ya maiti ya hiospitali ya Thika,familia ya jamaa huyo ilitarajia kuwa huenda angezikwa 3 jioni japo ratiba hiyo ikabadilishwa .

mwili uliwasilishwa usiku ukiwa na maafisa wa afya ambao waliendesha shughuli hiyo haraka wakiwa wamevalia magwanda ya kuwakinga dhidi ya maambukizi.

Aidha waziri wa afya kaunti ya Murang'a ameshutumu vikali uongzi wa hospitali ya Thika kwa kutuma ujumbe wakiwa wamechele kuwa mwathiriwa huyo alifariki kutokana na virusi hivyo hatari.